Ajira kwa watoto bado imetamalaki katika nchi nyingi za Kiafrika huku kilimo kikiongoza katika kuajiri watoto

Ajira kwa watoto bado imetamalaki katika nchi nyingi za Kiafrika huku kilimo kikiongoza katika kuajiri watoto

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Ajira kwa Watoto ni kazi ambazo huwazuia watoto kuishi katika utoto wao, kuwavunjia utu na heshima yao pamoja na kuathiri ukuaji wao wa mwili na akili. Zaidi ya hayo Ajira kwa Watoto ni zile ambazo huingilia masomo yao kwa kuwanyima fursa ya kuhudhuria shule; kuwalazimisha kuacha shule kabla ya wakati au kazi ambazo huathiri mahudhurio yao shuleni. Kazi hizi huweza kuwa hatari kwa afya ya mwili na akili ya mtoto. Mashirika mbalimbalina taasisi nyingine za haki za binadamu yakiongozwa na Shirika la Ajira Ulimwenguni (ILO) yanapambana kukomesha na kazi za aina hii kwa watoto.

Kumbuka kuwa tunaposema Ajira za watoto haimaanishi kila kazi anayopewa mtoto nyumbani au mtaani ni ajira za utotoni. Katika kufafanua zaidi jambo hili, Shirika la Ajira Ulimwenguni (ILO) wanaeleza kuwa si kila kazi zinazofanywa na watoto hupaswa kuchukuliwa kama ajira kwa watoto ambayo inapaswa kumulikwa na kukomeshwa. (ILO) wanabainisha kuna kazi ambazo zinaweza kuwafanywa na watoto lakini haziathiri afya zao au kuingilia masomo yao na huchukuliwa kuwa kitu chanya. Baadhi ya shughuli hizi chanya ni pamoja na kusaidia katika biashara ya familia, kupata pesa nje ya saa za shule au wakati wa likizo za shule. ILO wanaeleza Shughuli za aina hizi huchangia ukuaji wa watoto na ustawi wa familia zao; wanawapa ujuzi na uzoefu, na kusaidia kuwatayarisha kuwa wanajamii wenye tija katika maisha yao ya utu uzima.

TAKWIMU ZA HALI YA AJIRA KWA WATOTO ULIMWENGUNI
Kwa mujibu wa ILO wanaeleza kuwa takribani watoto milioni 152 , wenye umri wa miaka 5 hadi 17 ulimwenguni, bado wako katika ajira ya watoto. Kilimo ndiyo sekta inayochangia zaidi, ikichukua asilimia 71 ya ajira zote za watoto duniani, ambazo nyingi zinachukuliwa kuwa hatari kwa afya, usalama na maendeleo yao. Ajira hizi za mashabani zinadaiwa kutokea katika mashamba ya familia na wakati wa usafirishaji wa mazao. Tazama katika kielelezo kifuatacho:

1648195647031.png

Picha: Takwimu za Ajira kwa Watoto katika sekta ya kilimo Duniani

Chati hiyo hapo juu linaonesha takwimu za Ajira kwa Watoto maeneo mbalimbali ulimwenguni. Kwa takwimu hizo zilizotolewa na ECTL fOUNDATION, ILO na wengineo linaonesha Bara la Afrika ndilo eneo lililoathiriwa zaidi na ajira za watoto ambapo mtoto 1 kati ya 5 wanaohusika katika utumikishwaji. Bara la Asia na Pasifiki zinafuata kwa 7.4% ya ajira ya watoto na Amerika na 5.3%. Ajira ya watoto sio tu katika nchi za kipato cha chini, kwa hakika nusu ya watoto walioathirika wanaishi katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Takwimu inaonesha kuwa nchi nyingi za Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahara ina watoto wengi zaidi katika utumikishwaji wa watoto kuliko katika maeneo mengine ya dunia kwa pamoja. Kulingana na makadirio, watoto milioni 86.6 wenye umri wa miaka 5-17 walihusika katika utumikishwaji wa watoto katika eneo hilo kufikia mwaka wa 2020. Idadi hii iliongezeka kwa zaidi ya milioni 16 tangu 2016
 
Ni kweli lakini tatizo chanzo ni umasikini. Kama Serikali za kiafrica zimefanya juhudi gani kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja, maana watoto wanalazimishwa na mazingira, mfano wanaishi na bibi ambae ni mzee wazazi wote wamefariki
 
Ni kweli lakini tatizo chanzo ni umasikini. Kama serikali za kiafrica zimefanya juhudi gani kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja, maana watoto wanalazimishwa na mazingira, mfano wanaishi na bibi ambae ni mzee wazazi wote wamefariki.
Daah ni kweli ndugu yangu na hii ndiyo changamoto kubwa barani kwetu. Ndio maana kwenye takwimu hapo inaonesha kila mwaka hali inazidi kuwa mbaya.

Wakati mwingine ajira za Watoto Afrika ni kitendawili kisicho na jibu. Kikubwa tu kila mtu kwa uwezo wake ahakikishe anafanya juhudi binafsi kuwaokoa watoto katika mazingira magumu na hatarishi.
 
Daah ni kweli ndugu yangu na hii ndiyo changamoto kubwa barani kwetu. Ndio maana kwenye takwimu hapo inaonesha kila mwaka hali inazidi kuwa mbaya.

Wakati mwingine ajira za Watoto Afrika ni kitendawili kisicho na jibu. Kikubwa tu kila mtu kwa uwezo wake ahakikishe anafanya juhudi binafsi kuwaokoa watoto katika mazingira magumu na hatarishi.
Pia kuna hili za wazazi vijijini kuwaambia watoto wao wajaze majibu ya uongo kwenye mitihani ya hitima shule ya msingi Ili wasichaguliwe sekondari Wana waambia hawana uwezo wa kuwasomesha.Ili mabinti waje mijini kufanya Kazi za ndani,kwa ushahidi wa watoto wa majirani zao wanasaidiwa na watoto wao walioenda mjini kufanya Kazi za ndani.
Hapa ni suala la ujinga kwa wazazi
 
Pia kuna hili za wazazi vijijini kuwaambia watoto wao wajaze majibu ya uongo kwenye mitihani ya hitima shule ya msingi Ili wasichaguliwe sekondari Wana waambia hawana uwezo wa kuwasomesha.Ili mabinti waje mijini kufanya Kazi za ndani,kwa ushahidi wa watoto wa majirani zao wanasaidiwa na watoto wao walioenda mjini kufanya Kazi za ndani.
Hapa ni suala la ujinga kwa wazazi
Hili ni kweli kabisa kuna wakati fulani nilikuwa Mbeya niliambiwa kuna watoto wengi hasa wasichana wanaambiwa wajifelishe makusudi ili wasiendelee na masomo. Kuna haja ya kufanya semina nyingi vijijini hasa kipindi cha karibia na mitihani kuwahamasisha wanafunzi umuhimu wa kufaulu na kuendelea na masomo.
 
Juzi nipo bar usiku saa 4 akapita mtoto ukimkadiria ana miaka chini ya 10 ana karai la malimao anauza. Nilisikitika sana ikabidi niagize beer ningine ninywe.
 
Back
Top Bottom