Ajira mpya: Ushauri wa kuacha Kazi

Kwahyo mwanangu juzi tu apo ukapata? Duuuh hongera,nipe chaneli basi za pale k/koo za biashara uliyokuwa unafanya
 
Mimi mpango wa kuacha upo palepale japo nmeingia kwenye mfumo mwaka huu, ila ngoja nijijenge kwanza,baada ya miaka miwili nitakuja na feedback humu, siombi ushauri kwa mtu yeyote awe mzazi au nani, mateso kuyapitia sijaanza leo, siwez kuishi kwa 600k mpaka kufa kwangu,,
 
Mkuu km wife n mama wa nyumbani na umesema hapo town biashara ya nguo inalipaa kwann usifungue wife akasimamiaa na akawa anafata mzigo dar uku ww unaendelea kupambana na ajira na kusoma fursa zingine .
Asipokusikia hapa,analake jambo
 
Chukua mkopo sepa zako.

Wako wengi sana washawahi fanya hivyo na hakuna aliesumbua.

Mkopo unaochukua dhamana Yako ni hio kazi.

Pia mkopo huo kabla hujapewa hukatwa bima ya mkopo.

Kwa namna yoyote Ile ukiacha kazi benki itapata faida kupitia bima ya mkopo huo.

Ukiendelea na kazi itapata double profit.

Wewe sepa sehemu kama moyo wako haijaukubali au kutulia ni kama gereza.

Kapambanie unachikiona wewe siku ukifanikiwa mama Yako atakuelewa.

Akihoji sana mwambie the way moyo wako unavyojisikia.

Fanya unachokipenda sio nani na nani wanataka.

Kuna mwanangu mmoja nae alipangiwaga bush huko 2017 akakaa two years akavuta mkopo akasepa zake.

Until Leo hajawahi Rudi kule Yuko na mishe zake kitaa
 
Ajira gani hiyo uliyoipata bila kufanya interview?
 
Night shift uliyofanya wakati wa msoto ndiyo wizi au namna gani?

Vijana mna mihemko sana,kuna mwl mwenzio alikopa huku akaacha kazi kimyakimya kwenda machimboni kufadhili duara,akatemwa kwenye payroll na hela zikaisha bila hata kuambulia mia.

Kapambana tena kurudi kazini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…