Ajira mpya za walimu july 2015

Ajira mpya za walimu july 2015

engijape

Senior Member
Joined
Nov 8, 2014
Posts
178
Reaction score
97
habari za saa hizi wana javi. naomba maelekezo yenu kwa wale wenye uzoefu humu. Nimemaliza chuo 2012 na nikapangwa kazini 2013 wilaya ya Rungwe. sikuweza kuripoti kwa sababu ya matatizo. mwaka jana nikatuma barua Tamisemi lakini sikupata ajira ya mwaka huu. Je , nilikosea kutuma Tamisemi au nilitakiwa nitume wapi. na mpaka sasa nataka kufanya maombi tena lakini sijui process. Pia ninaweza kurudi kituo changu cha kwanza cha kazi??? Asanteni sana wadau.:cheer2::cheer2::cheer2:
 
Kwanza kitendo cha kutokwenda kuripoti inaonesha kuwa hupendi na hutaki aina hiyo ya kazi kwahiyo kila ukituma wakiingiza jina lako kwenye mfumo linaonekana kuwa uliwahi kupangwa kituo ukakaidi kamwe hutapangwa labda nenda wizara ya elimu wakupe utaratibu wa kufuata then nenda tamisemi ujieleze baada ya hapo watakujumuisha lakini baada ya maelezo marefu sana.
 
Hakuna kosa kubwa kwenye utumishi wa umma kama kupangwa kituo halafu ukaacha kwenda kuripoti bila tarifa.
 
Asante sana ndugu yangu kwa ushauri wako ila sikukataa kuripoti kwa sababu siipendi ualimu. kilichotokea ni shida ambayo isingeepukika. Pia sikuripoti kabisa kwa sababu ningeripoti ningerudi kituo changu cha kazi. naendelea kuomba ushauri kwenu wadau na mwisho wa siku nitafanikiwa kupitia mawazo yenu wadau. Asante.
 
Teh pole ulipata dili lingine afu limebuma nini? Nenda wizarani kapate mwongozo
 
Heading yako haiendani na maelezo uliyotoa. Hilo suala linawezekana. Wengi huwa wanapangiwa tena. Cha msingi fika wizara ya elimu idara kwenye yako kama sec au pri jieleze utafanikiwa2 mana nawajua weng wenye tatizo kama lako na now wamepangwa upya.
 
Back
Top Bottom