Pre GE2025 Ajira na majanga yake kwenye siasa, mwenye sikio na asikie

Pre GE2025 Ajira na majanga yake kwenye siasa, mwenye sikio na asikie

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

kacnia

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2014
Posts
4,024
Reaction score
15,796
Naandika haya nikiwa na uchungu mkubwa, sina hata muda wa salamu maana tutachoshana tu.

Nilikua nikisikia maafisa wa serikali wanashauri vijana tujiajiri, nilidhani ni wanafiki, kumbe wanapitia magumu sana na hawatamani wengine yatukute, ila sasa walishakua walemavu wa fikra hawana kimbilio zaidi ya kutegemea pesa za mwisho wa mwezi na posho pamoja na janja janja wanajikuta hawana namna zaidi ya kuvumilia fedheha, dharau manyanyaso na mateso kwa boss wao, (kuhusu bata ni juu yao, wote tunakula bata kwa namna yetu)

Imagine mtanzania mwenzetu anapitia vipindi kama hivi
GTCYLlrWMAAdYsT.jpeg



Hapo haujazungumzia spana anazo kutana nazo huko x na mitandao mingine ya kijamii.

Ninachoweza kumshauri mh: AJIAJIRI.

binafsi nilipogundua kumbe ukiwa umeajiriwa siku ukipishana tuu na kimada wa bosi unapoteza umuhimu wako kama mfanyakazi na hatimaye kutafutiwa sababu ya kufukuzwa licha ya juhudi unazoweka kikazi. Nilihamia kwenye biashara ya matunda.

Mh: ikitokea umetenguliwa ili uhamishwe wizara au upande cheo, usinisahau, maana kujiajiri nako ni mtiti kama hauna mtaji.

Semaji la ma jobless!

Pia soma: Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
 
Asante sana, hili mchanganuo wake
2000-sportpesa
1000- wali maharage mchana
1000-wali maharage usiku
1000-maji ya uhali lita 1.6

2000- kibubu
1000- internet bundle mb 490 za wiki (ila zinatumika masaa matatu)
2000- natunza ili kesho yake nisife njaa.

Maisha chini ya dollar moja ni mtiti
GSpJtpQWkAAk7Bn.jpeg
 
Back
Top Bottom