MWANAHARAMU
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 4,041
- 10,699
Mfumo wa elimu yetu hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla, umeandaliwa kuandaa kundi la watu ambao wataajiriwa.
Hivyo kupelekea kutengeneza kundi kubwa la Vijana wasio na ajira kutokana na ushindani kuongezeka, huku nafasi za ajira zikiwa finyu kila mwaka.
Ila leo hatuangalii hili kundi bali, tunatazama kwa muono mpana hali ya watu walioajiriwa na Umasikini.
Kipi hasa hupelekea walioajiriwa kukabiliwa na hari ya Umasikini.
1) UFINYU WA ELIMU YA FEDHA
Kumbuka huyu mtu kasoma miaka yote kumudu aina fulani ya utaalamu.
Mfano: Daktari hivyo atafanya kazi miaka yake yote kwenye Taaluma ila bado ataingia kwenye lindi la Umasikini kwa sababu ya kutokuwa na elimu na akili ya fedha.
2) UKOSEFU WA MUDA
Kwa mtu aliyeajiriwa huutumia muda wake mwingi kazini badala ya ama kuanzisha au kusimamia miradi yake hivyo biashara nyingi za waajiri hugs mapema au kujiendesha kwa hasara.
Mfano: Bwana Mahenge hutumia masaa tisa au kumi alipoajiriwa.
3) UKOSEFU WA VYANZO MBADALA VYA MAPATO.
Hapa ndio Kuna Ile Shida maana mtu atautegemea pesa ya ujira au mshahara wake mmoja mpaka mwingine, ambao kiukweli hautoshelezi mahitaji.
4) WOGA WA KUWEKEZA NA IMANI POTOFU
Ipo Imani miongoni wa watu kuwa kuwekeza ni kupoteza fedha zako, hii ilitokea baada ya makampuni kufirisika na mitaji ya watu kwenda na maji.
Mfano: kampuni ya DECI na jinsi ilivyoliza Watanzania baada ya kujulikana ni utapeli mweupe.
5) PENSHENI NA KIINUA MGONGO
Waajiriwa wengi wamelidhika na kuamini kwamba pesa yao ya kiinua mgongo itawafuta jasho uzeeni na kuendelea kuishi maisha yao ila ni kitu ambacho sio kweli.
Mfano: Waajiriwa walioajiriwa kabla ya mwaka 1995 wanapata 20,000 kama pensheni, je hii inawatosha kwenye Matumizi ya mwezi?
6) UKOSEFU WA MTAJI
Kuna mtaalamu mmoja wa maswala ya fedha aliwahi kusema, tatizo la Waajiriwa sio mtaji ila Nia ya kufanya uwekezaji.
7) KUTOKUWA NA NIA
Ndiyo unaweza ukawa na kila kitu yaani mtaji, muda ila ukikosa nia hautoweza kufanya uwekezaji au biashara kujiendesha na kuleta faida.
8) KUNUNUA VITU VYA ANASA MWANZO
Mtu anapopata ajira mwanzoni hasa hapa Tanzania basi ukimbilia kununua vitu vya anasa badala ya kuwekeza ili kuimarisha hali yake kiuchumi.
Mfano:Wanajeshi wengi hukimbilia kununua Magari binafsi ya kutembelea ambayo yanawatoa fedha kulihudumia hivyo kuzidi kujiingiza shimoni.
9) KUCHUKUA MIKOPO ISIYO NA TIJA
Jamani hili ni linasumbua kweli kweli hasa Waajiriwa ambao huchukua mikopo bila ya kuwa na mpango mkakati jinsi ya kutunisha fedha zake.
Mfano: Walimu ambao huchukua mikopo bila ya kuwa na mipango thabiti
Nisikilizeni Waajiriwa wawe wa Serikari au Sekta binafsi kumbukeni muda wa kuandaa maisha yako ya uzeeni ni Sasa kwa kuwekeza na ujiandae kuishi bila kuitegemea Serikari.
Siku zote kumbukeni Wazee wa Afrika Mashariki kilichowakuta

Upvote
0