KERO Ajira Portal wapo kweli ofisini? Dawati la msaada ambalo halisaidii kitu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
NAOMBA MSAADA KWA ANAYEJUA NAMNA YA KUWAPATA. Nahitaji sana huduma yao.

Nimefungua Akaunti ya Ajira Portal, na nimetumiwa email na link ya ku-activate account yangu lakini kila niki-click ile link kwenye email yangu, link haifunguki. Nimeawaandikia email lakini hawajajibu. Nimewapigia simu hawapokei.

Naombeni msaada tafadhali.
 
Nahisi hawapo ofisini maana simu zao zinaita tu
 
Kama upo Dodoma nenda ofisini kwao watakusaidia.

Siku hizi Bongo ofisi za umma hawana msaada hata wa kupokea simu
 
Aise Ni kwel hawa jamàa awajibu chochote
 
Kwanza kabisa naipongeza Serikali ya Jamhuri ya muungano Tanzania kuamua ajira zote ziombwe kupitia mfumo mmoja wa kidigital wa AjiraPortal.

Changamoto kubwa kwa baadhi ya waombaji ajira kupitia mfumo huu ni namna ya kuutumia mfumo huo, hali hii inapelekea waombaji kuhitaji msaada zaidi kwa watoa huduma kwa wateja.

Kero inakuja pale umepata changamoto na unahitaji msaada kwao, unawatafuta na kuwaelekeza shida zako lakini wanakuwa SIO MSAADA na Muda mwingine hawajibu emails kabisa.

Nafasi za ajira zinatolewa ambazo tunasifa nazo kabisa lakini tunashindwa kuziomba hadi deadline inafika tunazikosa. Hatuna pakusaidiwa kwani Huduma kwa Wateja sio MSAADA.

Naomba Serikali isikie kilio chetu, maana tumechoka kukaa mtaani. Waweke namna nzuri kwa sisi tunaopitia changamoto tuweze kusaidiwa.

INAUMA SANA NAFASI INATOLEWA NA UNASIFA YA KUIOMBA LAKINI UNAISHIA KUIANGALIA TU KWASABABU HAUWEZI KUFANYA CHOCHOTE.
 
Msaada Kwa mdogo wangu amesahau username na password kwenye ajira portal system kwa anaeweza nisaidia kutatua hili
Tumejaribu kuwapigia simu hawapokei na deadline ya nafasi za KAZI imekaribia
Na vipi inawezekana kuifuta account na kufungua mpya?
 
Msaada Kwa mdogo wangu amesahau username na password kwenye ajira portal system kwa anaeweza nisaidia kutatua hili
Tumejaribu kuwapigia simu hawapokei na deadline ya nafasi za KAZI imekaribia
Na vipi inawezekana kuifuta account na kufungua mpya?
Awatumie email na asiache kupiga simu watamsaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…