Kupata kazi ni haki ya kila raia mwenye sifa STAHIKI kwa miongozo ya kitaifa na kimataifa. Sifa kubwa ni kuhitimu katika fani inayotakiwa sokoni kutoka kwenye vyuo vinavyotambulika na mamlaka za nchi husika.
Kama tunavyotambua safari ya masomo/elimu ni safari ya kujitoa kwa mali, muda na hali. Ni uwekezaji wa gharama na wa muda mrefu ambao unatarajiwa kuwa manufaa baada ya kuhitimu hasa kupitia ajira (kuajiriwa/kujiajiri). Kwa nchi yetu ambayo iko kwenye orodha nchi maskini au mara chache kuingia uchumi wa kati chini, elimu huziacha familia kwenye umaskini mkubwa baada ya kutumia rasilimali nyingi kufadhili elimu ya mtoto au watoto wao.
Mitaala yetu kwa kiwango kikubwa ni ya kuwawezesha zaidi wahitimu kujiariwa kuliko kujiari. Pamoja na uchache wa nafasi zilizopo serikalini, kupata nafasi hizo umekuwa ni uwekezaji mwingine ambao unaonekana kuwa ghali na wenye mateso kuliko elimu yenyewe. Matumizi pesa kusafiri, muda na usumbufu mwwingine.
Ajira kwa fani nyingi zimekuwa zikitolewa kwa mfumo wa usaili ambao ni kitu kizuri kupata wahitimu mahiri kuendana na kasi na ufanisi wa mahitaji ya huduma kwa wananchi lakini zoezi hili limekuwa kichaka cha kujificha kwa vyuo visivyo na sifa. Kumekuwa na changamoto kubwa ya waajiri na jamii kulalamikia uwezo mdogo wa wahitimu kutoka vyuoni kinyume na ilivyotarajiwa. Mamlaka iweke nguvu ya ziada katika kudhibiti ubora wa vyuo na kuboressha mitaala kuliko kudhibiti wahitimu kupitia usaili ambao huenda walitapeliwa na vyuo visivyo na sifa.
Kutokana na changamoto hiyo suluhu ya kudumu kwenye kupata watumishi wa umma iwe kama ifuatavyo;
Wahitimu wote kwenye vyuo vinavyotambuliwa na serikali wawekwe moja kwa moja kwenye kanzi data ya serikali inaweza kuwa ajira portal. Kila nafasi zikipatikana kwenye vyeo vya chini vya fani husika, wahitimu wa fani hiyo wapangiwe vituo vya kazi na kwa maslahi (mshahara) ya vyeo hivyo vya chini bila ya usaili na bila kujali kiwango cha elimu cha wahitimu. Mfano mwalimu wa shahada anayestahili kufundisha sekondari au zaidi apangiwe kufundisha msingi au wanafunzi wanaohitaji mwalimu wa ngazi ya astahahaha au stashahada kwa mshahara huo huo wa cheo cha nafasi iliyopo.
Upangaji wa nafasi za kazi uzingatie kigezo cha mwaka wa kuhitimu na umri. Nafasi kwenye vyeo vinavyofata kwa fani husika ndizo vitokane na usaili kwa wenye sifa waliokazini (transfer vacancies). Watu wapande vyeo vya juu na huku chini wengine waingie moja kwa moja (by default).
Nafasi zinazoachwa wazi baada ya usaili, nafasi hizo zijazwe moja kwa moja (by default) kutoka kwenye kanzi data ya wahitimu wanaosubiri ajira. Itakuwa rahisi kwa wahitimu kuweka matarajio ya ni lini atafikiwa kupitia kanzidata husika ambayo kila mhitimu ataweza kuwa akaunti huko.
Kwa sababu tayari serikali imetangaza kuendesha usaili wa mchujo wa kuandika (written) kwenye vituo mbalimbali karibu kila halmashauri kwa njia ya mtandao hivyo kuwa rahisi mwombaji aliyekazini kupata nauli na ruhusa ya siku moja au mbili kuhudhuria usahili huo wa mchujo. Kama mpango wa usaili kimtandao kila halmashauri bado HAUJAKAMILIKA basi uharikishwe.
Hii itasaidia serikali kutumia vizuri rasilimali watu, kupunguza gharama kubwa za usafiri na usumbufu kwa wahitimu. Pia serikali itawajibika kuhakikisha vyuo vinatoa wahitimu wanaofikia umahiri unaotakiwa kuliko KUWAKWEPA WAHITIMU kupitia mgongo wa usaili ambao umegeuka mateso. Inaumiza sana mhitimu kukaa mtaani kwa kigezo cha kuwa na sifa za juu (OVER qualified) au kushindwa USAILI kwa miaka zaidi ya mitano huku waliohitimu baada yake wakiwa wanapata kazi. Tukumbuke kwenye saili kuna mambo mengi kuanzia kusahau mambo muhimu baada ya kukaa uraiani kwa muda mrefu, uwezo wa mhusika kujieleza, makosa ya kibinadamu, yasiyo ya kibinadamu na mengine mengi.
Mtindo huu wa utoaji ajira serikalini utasaidia waajiriwa kuwa wakijiendeleza (updated) wakiwa kazini kwa njia mbalimbali kama vile mitandao ili kujiweka kwenye nafasi nzuri za kupata nafasi kwenye vyeo vya juu vya fani zao. Pia kuwa na watumishi wenye sifa za ziada kwenye vyeo vya chini kutaongeza ufanisi kwenye nafasi za chini walizonazo kwa wakati huo huku wakishirikiana na kubadilisha ujuzi na uzoefu na wafanyakazi wenzao.
Aidha nadharia hii italeta msawazo wa kifikra kwa vizazi vyetu, wa kuwa hatua ya KWANZA kazini kwa WOTE NI SAWA na kupanda kwenda juu (cheo/maslahi) ni jitihada binafsi za ziada za kielimu, ufanisi na uzoefu kazini.
Tukumbuke mahitaji ya msingi kwa binadamu wote ambayo ni chakula, malazi na mavazi ni sawa hivyo si ajabu mhitimu wa shahada, umahiri au uzamivu kuanza na cheo chini ya elimu yake (maslahi ya chini) ili kumudu mahitaji ya msingi ya kila siku huku akisubiri nafasi za juu kulingana na sifa alizonazo.
Pia tukumbuke elimu ni kwa ajili ya kuhudumia jamii zetu kwa ufanisi, pamoja na kwamba mshahara kulingana na elimu ya mtu ni HAKI ila utendaji kazi na kulinda UTU wa wahitimu ni kwa maslahi ya jamii na Taifa. Kipindi ambacho nafasi kulingana na elimu ya juu ya wahitimu waliyonayo hazipatikani basi ni vizuri wahitimu hao wakatumika kwa maslahi ya Taifa kwenye nafasi za chini ili kulinda utu wao wa kupata mahitaji yao ya msingi kwa kumpa nafasi za kazi zilizopo na maslahi yaliyopo. Wahitimu wanaohudumia nafasi za chini kulingana elimu zao wapewe unafuu fulani mfano kutokatwa mikopo ya elimu ya juu mpaka watakapofikia MASLAHI wanavyostahili kulingana na elimu yao.
HIYO NDIO TANZANIA TUITAKAYO.

Upvote
1