Ahmed Saidi
JF-Expert Member
- Oct 15, 2019
- 1,588
- 3,487
Kwanza niaze kwa kumshukuru Mola mlezi kwa kila neema na upendo wake.
Natumai wote ni wazima. Nianze tu kwa kuipongeza serikali kwa kuajiri watumishi wapya katika sekta ya elimu na afya, kiukweli serikali kupitia OR-TAMISEMI imejitahidi kutenda haki kwa namna mchakato mzima ulivyofanywa ili kuajiri watumishi hao.
Siwezi kuwasemea wengine ila wengi tumeridhika na jinsi utaratibu ulivyoenda kuwaajiri waalimu na wataalamu wa afya ingawa hata mwenyewe sijapata nifasi hiyo. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, hongera serikali yetu.
Siku za nyuma kidogo niliweka chapasho hapa kuhusu namna nzuri ya kuajiri watumishi bila malalamiko, sitaki kusema serikali ilisoma ule uzi wangu ila ni kama wamefanya nilichokiandika. Katika ajira hizi serikali imewapa kipaumbele waliomaliza masomo yao miaka ya nyuma kidogo na sisi wapya wapya tukae kidogo mtaani tujifunze maisha ili hata siku tukipata nafasi basi tusisahau na wengine. Unakuta mtu anamaliza chuo leo kesho anapata kazi na kuwaacha kaka na dada zake waliokaa mtaani muda mwingi, hii inawakatisha tamaa hao waliokaa mtaani na huyu aliepata kiurahisi hawezi jua maana ya maisha magumu.
Pia serikali imewapa kipaumbele wale wenye masomo yanayoitajika sana (science), hili ni Jambo la msingi sana kuliko wangetumia kigezo cha kujitolea ambapo wengi wenye masomo ya science hawajitolei Jambo ambalo lingeongeza waalimu wa sanaa mashuleni ambapo mahitaji yao si makubwa sana.
Kubwa ajira hizi zimetupa imani kuwa ipo siku hata sisi tulio mtaani tutakumbukwa, ingawa watu bado ni wengi sana. Kama serikali itaajiri kwa kuzitia muda wa muombaji aliohitimu basi bila shaka hata mimi zamu yangu itafika.
Hongera wa waliopata nafasi, ila sisi ambao hatupata tusikate tamaa, maisha yapo bado, tuendelee kupambana. La msingi tuendelee kutafuta, hata iwe tunapata Mia, Mia mbili hicho hicho Mungu ndio katujaalia, huwezi jua huenda iyo ndio njia ya kufanikiwa, kwani wangapi wamepata mafanikio makubwa mbali na ajira hizi za serikalini na hata ikatokea ukapata ajira basi utakuwa unakitu fulani umekiwekeza na utakiendeleza. Tusikate tamaa, Mungu yupo nasisi, tumkumbuke Sana yeye, tumuamini, tufanye sana ibada na tujikite katika kutenda mema.