Ntiyakama
Member
- Sep 19, 2021
- 32
- 37
Kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya mwaka 2012 asilimia 77% ya watanzania wanaumri chini ya miaka 35 na asilimia 19% kati ya hao wanaumri wa miaka kati ya 15 – 24.
Kiasi cha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana hao (wenye umri kati ya mika 15 – 24) ni asilimia 13.4% ambapo hali ni mbaya zaidi kwa vijana wa kike (asilimia 14.3%) ukilinganisha na vijana wa kiume wa umri sawa na huo (asilimia 12.3%).
Utafiti uliofanywa na shirika la ‘restless development’ nchini Tanzania mwaka 2012-2013 ukihusisha jumla ya vijana 1037 kutoka mikoa ya Dodoma (Bahi), Arusha (Monduli), Rukwa (Sumbawanga), Shinyanga (Kahama), Ruvuma (Nyasa), Dar es Salaam (Ilala) na Mwanza (Magu), ulionyesha 50.2% hawajaajiliwa wala kujiajili, 1.9% wanafanya kazi za muda mfupi (part-time), 2.2% wameajiliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali, 1.5% wameajiliwa Serikalini, 3.8% wameajiliwa katika sekta binafsi, 4.8% wamejiajili sekta nyinginezo, 16% wafanya biashara, 19.3% wamejiajili katika kilimo.
Inaweza kuwa ngumu kidogo kupata kilicho kusudiwa katika ripoti hiyo kwasababu ya kutokupata nini maana ya asilimia hizo kwa haraka: hii ina maana kati ya vijana 1037 waliohusishwa kwenye utafiti; vijana 520 hawakuwa na kazi yeyote!
Vijana 18 wanafanya kazi za muda mfupi, vijana 29 wameajiliwa na mashirika binafsi, vijana 15 tu ndio walioajiliwa Serikalini! 39 wameajiliwa katika sekta binafsi, 50 wamejiajili sekta nyinginezo, 166 ni wafanya biashara na 200 wamejiajili katika sekta ya kilimo.
Ni watu 15 tu kati ya 1037 (1.5%) ambao wameajiliwa serikalini, mahala ambapo kundi kubwa la vijana ikiwemo wahitimu wengi wa vyuo na vyuo vikuu, wanaitazama kama sekta pekee inayoweze kuwaajili na kuwapatia maisha mazuri!
Kwa sababu ya kuelekeza fikra na mawazo yote serikalini ambako kuna nafasi chache zaidi vijana wengi wakiwemo wanaohitimu vyuo na vyuo vikuu hufunga mitazamo na fikra zao kuelekea kujiajili hivyo kubaki bila kazi (50.2% wasio na kazi!).
Vijana waliofanikiwa kufika mashuleni, kusoma mpaka vyuo na vyuo vikuu, wanatazamwa kama walio elimika ambapo ni matarajio ya wengi kuwa wanaweza kuitumia elimu waliyoipata kwa manufaa ya wengi.
Ni kinyume kabisa na mtazamo huu kwani wengi wao wemekuwa wasio na msaada tena wasiofaa kwa lolote katika jamii zao (ukilinganisha na wale ambao hawakufanikiwa pengine kwenda shuleni kabisa), hasa pale wanapokosa kuajiliwa katika taaluma walizokuwa wakizisomea.
Zaidi sana wengi wao wanakuwa hawawezi kushiriki baadhi ya shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wenzao ambao hawakufanikiwa kupata elimu shuleni.
Ni wazi kwamba baadhi ya vijana wanaohitimu vyuo hughubikwa na mtazamo wa kujitenga, kujibagua, kwa kujiona ni wathamani na bora zaidi kuliko wenzao wengine ambao hawakwenda shule; kwasababu hii hujitenga na wenzao na kuwapelekea kushindwa kushiriki shughuli za kiuzalishaji katika jamii zao, wakibaki kusubiri ajira Serikalini.
Kwa sababu hii, hakuna kinacho wafaidia kutokana na digrii wanazo tunukiwa hasa pale kunapo kosekana ajira serikalini, kitu ambacho ni tazamio lao la kwanza.
Tuelekeze fikra zetu katika kujiajili ndani ya sekta mbalimbali; kilimo, biashara, uvuvi, ujenzi, viwanda vidogovidogo, ufugaji, n.k
Lazima uhisi na uone kuwa unawajibika kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, usibaki kufikiria tu kwamba serikali hakuna inachokifanya kwa ajili yako; jifunze kusimama ulipo vyema, kutumia ulichonacho na kufanya kikupasacho vyema, kisha amua kutumia uwezo wako kwa ajili ya manufaa yako naTaifa kwa ujumla.
Pengine lile unaloliona limekwama, halifanyiki kwa sababu wewe ni mmoja kati ya waliopaswa kulitekeleza lakini bado hujalitelekeza ukisubiri serikali ilifanye kwa ajili yako.
Unawakwamisha wengi. Chukua hatua.
Marejeo;
1. 2012, Sensa ya Watu na Makazi. Ofisi ya Takwimu ya Taifa
2. MKUKUTA, Taarifa juu ya umaskini na maendeleo ya Watu, 2011
3. Youth in Tanzania today: Restless riport, 2012/13

Upvote
0