WIZARA ya Kilimo, Chakula na Ushirika imetangaza nafasi 574 za kazi katika fani mbalimbali zinazohusu sekta ya kilimo na idara zake.
Nafasi hizo zinawalenga watu wenye sifa mbalimbali ikiwemo kuwa na umri usiozidi miaka 45 na elimu ya kuanzia Shahada moja na kuendelea kulingana na aina ya kazi.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwa vyombo vya habari juzi na Ofisi ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, waombaji wenye sifa wanapaswa kupeleka barua za maombi katika ofisi yake na wawe tayari kupangiwa kazi wizarani na ofisi za mikoani za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Eneo lenye nafasi nyingi za ajira ni Ofisa Kilimo Daraja la II ambapo ajira 378 zitatolewa kwa waombaji wenye sifa za kuwa na Shahada ya Sayansi Kilimo na Mazingira, nafasi zote zikihitaji wahitimu kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambulika na Serikali.
Aidha, ajira 70 zitatolewa kwa Ofisa Utafiti Kilimo Daraja la II ambapo waombaji wanapaswa kuwa na Shahada ya Kilimo, Uchumi Kilimo, Uhandisi Kilimo, Sayansi ya Chakula na Teknolojia, Sayansi ya Viumbehai na Maabara, Udongo na Mazao (Agronomy), Mazingira na Mazao ya Bustani na Maua.
Nafasi nyingine 88 ni katika Uhandisi Kilimo Daraja la II na kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji wawe na shahada ya Uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya kilimo, umwagiliaji, ujenzi, ufundi na mazingira.
Ajira 38 ni za Mkufunzi Kilimo Daraja la II ambapo waombaji watapangiwa kuwa wakufunzi katika vyuo vya kilimo na mifugo vilivyo chini ya Wizara ya Kilimo na ile ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na wanahitajika watu wenye Shahada katika kilimo kutoa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) au kingine kinachotambulika na Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara, waombaji wanapaswa kupeleka barua zao siku 14 kuanzia taarifa ilipotolewa katika vyombo vya habari.
source: Habari leo 10.11.2011