Hii ni hatari kubwa kwa vijana wa leo:-
Migodini wamejaa makaburu, wazungu.
Kwenye biashara (eg KKoo, gereji, viwanda vidogo etc) wamejaa wachina.
Kwenye makampuni ya ujenzi wa majengo na barabara wamejaa wachina.
Kwenye makampuni ya simu (eg Voda, Airtel etc) wamejaa Wahindi na wanaongezeka kwa kasi.
Kwenye stationery kubwa na maduka ya computer used eg kariakoo na city center wamejaa Wasomali.
Kwenye ardhi nono ifaayo kwa kilimo vijijini wamechukua Wawekezaji.
N.k, n.k, n.k
Enyi watu wa uhamiaji, uwekezaji, watoa vibari vya kazi amkeni kutoka katika usingizi huo mzito mliolala.
Hii mianya mnayoiachia inaumiza watanzania na jamii ambayo hata ninyi mmo ndani yake.
HRs na maafisa mbalimbali wa serikali simamieni haki, taratibu na sheria ili kunusuru jamii yetu hasa vijana wengi wanaosoma na kumaliza vyuoni.