Ajira za Ualimu: Je, Masomo ya biashara hayafundishwi mashuleni?

Ajira za Ualimu: Je, Masomo ya biashara hayafundishwi mashuleni?

KAUCHEZEA

Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
29
Reaction score
15
Ajira za Ualimu zimetangazwa na Vijana wengi wameanza kuchangamkia Ajira ili waende kulitumikia Taifa na kuendeleza taaluma zao, lakini Walimu waliopewa kipaumbele ni Walimu wa Sayansi, Hesabu na Mengine Kidogo.

Ila Walimu wa Masomo ya biashara yaani Book Keeping na Commerce wametengwa kabisa na bado wapo mitaani Kama wengine.Lnk Asilimia kubwa watoto wengi wanakutana na Masomo haya wanapokwenda vyuo vikuu na kukosa Misingi na ujuzi wa Masomo haya pindi wanapotaka kuwa wahasibu au kupata ujuzi kidogo wa kuweka rekodi ya fedha na kujua vizuri nyaraka za biashara.

Miaka ya 90 kwenda mbele Watoto wengi walikuwa nawapenda sana Masomo haya mpaka leo leo kwa sasa wengi wanayakimbia baada ya kukosa Walimu mfano wa shule zilizokuwa zinafanya vizuri kwa Masomo haya ni Kibaha SC, Azania, Kibasila, Umbwe Sec ,Nk.

Tunaomba Wizara husika muwafikilie Walimu hawa kwani wanahitajika sana kwenye kulijenga Taifa.
 
Ukweli inashangaza sana kuona masomo ya msingi kama haya yakitumipiwa kisogo namna hii .
 
Back
Top Bottom