Ajira za ualimu mwaka huu zipo au hazipo?

Ajira za ualimu mwaka huu zipo au hazipo?

Masculinity

Member
Joined
May 6, 2024
Posts
16
Reaction score
15
Kiukweli nashangaa sana viongozi na roho zetu binadamu hivi kwann mtu akifanikifanikiwa anasahau maisha ya wenzake hata kama amesota nae au nao?

Ndg zangu hivi serikali inafikiliaaje walimu walioko mtaani waliomaliza vyuo naona kama wanaona ni watu ambao hawatambuliki na serikali kabisa. Just imagine mwaka unaenda kuisha na hakuna chochote wanachojua juu ya hatima yao kuwa mwaka huu hakuna ajira au hakuna?

Hii inamaanisha taifa kwa upande wa walimu either hakuna msemaji wao au mtetezi wao sababu ajira za ualimu tumezoea mwezi wa saba watu wana-report kazini lkn mwaka huu sijui ndo hakuna ajira za walimu.

Ni bora kila mwaka muajiri hao wachache watazid kufariji wenzao kuwa ajira zipo lakini mkianza kuwaona kama wao mazoba mnakuwa mnakosea sana wakati nikifatilia sana taifa ili wasomi wengi ni walimu.

Naone kizazi cha uongozi kijacho sababu kisipoangalia kitakuta taifa ili liko kama Kenya au Congo
 
Swali: Serikali inaajiri kada fulani ili kukidhi uhitaji wa kukidhi mahitaji ya wasomi wa kada hiyo?
Kada za ualimu miaka na miaka mmebebwa sana, mmeajiriwa kwa mafungu au kwa ujumla, hamjafanya usaili sasa hivi mambo yamebadilika kidogo tu kijasho kinawatoka.
Tulieni.
 
Atulize wenge
 
Kama unasubiri ajira subiri huku ukiwa unajipambania kwa plan B ,ngumu kukubali ukweli mchungu kwamba elimu ni kwa ajili ya kutatua changamoto kwenye mazingira yetu sio kuajiriwa .Sisi ilitukuta hii 2016 saiv nishazoea sihitaji kuajiriwa .
 
Back
Top Bottom