msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Miongoni mwa mambo yanayotakiwa kutupiwa jicho ni ubaguzi uliopo kwenye utoaji wa ajira kwa kada mbali mbali ikiwemo ualimu
Serikali ya awamu ya tano chini ya utawala wa hayati Magufuli imekuwa ikitoa ajira za ualimu kwa upendeleo na ubaguzi bila kuzingatia usawa na elimu za waombaji
Tumeshuhudia kwa miaka mitano mfululizo walimu wenye elimu ya shahada 'degree' wakibaguliwa wazi wazi kwenye mchakato wa ajira. Si walimu wa sanaa wala wa sayansi wote kwa ujumla wao wamesomeshwa namba vyakutosha huku kipaumbele cha ajira wakipewa walimu wa cheti na stashahada pekee
Kwakuwa utawala umebadilika, chini ya Rais wa awamu ya sita mama yetu Samia Suluhu Hassan tunaamini serikali yake itaenda kufanya mabadiliko makubwa kwenye utoaji na upangaji wa ajira ili walimu wote bila kujari elimu zao waajiriwe kwa uwiano sawa bila ubaguzi wowote wa kielimu.
Hali hii imekuwa ikiwakatisha tamaa vijana wengi wenye elimu ya shahada kuomba ajira kwa sababu hata wanapoomba wanakuwa hawana matumaini ya kupata kwani kuna imani imejengeka kwamba serikali haiwaajiri ili kubana matumizi ya bajeti hususani kwenye upande wa mishahara.
Sasa basi ili kuondoa dhana hii Tunaiomba serikali itakapotangaza ajira 6000 za ualimu hivi karibuni ije na majibu ya kueleweka juu ya walimu wangapi wa shahada 'degree' iliyowaajiri ili kusudi kama idadi itakuwa ni ndogo basi vijana wajue namna ya kujipanga kufanya mambo mengine kuliko kupotezewa muda wao kuomba ajira ambazo hawaajiriki..!
KAZI IENDELEE....