Mnyalu Junior
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 573
- 199
Baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye ajira za ualimu zimetoka. Ingawa wengi wamepelekwa vijijini lakini kutoka kwa ajira hizo kumeleta matumaini na furaha mpya kwa wahitimu wote waliokuwa wanasubiri ajira kwa hamu kubwa
Hali imekuwa tofauti kwa wahitimu wa chuo cha Sebastian Kolowa Memorial University baada ya kuchungulia majina yaliyotolewa na kutoona majina yao!
Chuo cha Sebastian Kolowa Memorial University kipo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga. Ni chuo pekee Tanzania kinachotoa "Elimu Maalumu". Elimu maalumu ni elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu kama vile Wasiosikia/Viziwi (Hearing Impairment), Wasioona (Visual Impairment), Wenye mtindio wa Ubongo/Usonji (Cognitive Disability and Autism Spectrum) na Wenye matatizo ya kuzungumza (Speech Impairment).
Wahitimu wa chuo hicho tupo njia panda na hatujui cha kufanya kwani majina machache yaliyowekwa ni ya wahitimu wa mwaka wa nyuma na tayari walishaajiriwa mwaka jana. Tunajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu;
Je, majina yetu hayakwenda TAMISEMI?
Je, TAMISEMI imejichanganya kwa kuweka tena majina ya wahitimu waliokwishaajiriwa?
Je, hatuna sifa ya kuajiriwa?
Wadau tunaomba ushauri tujue nini cha kufanya.