Ajira za ualimu zimetoka lakini SEKOMU Hakimo

Mnyalu Junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2012
Posts
573
Reaction score
199
Baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye ajira za ualimu zimetoka. Ingawa wengi wamepelekwa vijijini lakini kutoka kwa ajira hizo kumeleta matumaini na furaha mpya kwa wahitimu wote waliokuwa wanasubiri ajira kwa hamu kubwa

Hali imekuwa tofauti kwa wahitimu wa chuo cha Sebastian Kolowa Memorial University baada ya kuchungulia majina yaliyotolewa na kutoona majina yao!

Chuo cha Sebastian Kolowa Memorial University kipo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga. Ni chuo pekee Tanzania kinachotoa "Elimu Maalumu". Elimu maalumu ni elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu kama vile Wasiosikia/Viziwi (Hearing Impairment), Wasioona (Visual Impairment), Wenye mtindio wa Ubongo/Usonji (Cognitive Disability and Autism Spectrum) na Wenye matatizo ya kuzungumza (Speech Impairment).

Wahitimu wa chuo hicho tupo njia panda na hatujui cha kufanya kwani majina machache yaliyowekwa ni ya wahitimu wa mwaka wa nyuma na tayari walishaajiriwa mwaka jana. Tunajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu;

Je, majina yetu hayakwenda TAMISEMI?

Je, TAMISEMI imejichanganya kwa kuweka tena majina ya wahitimu waliokwishaajiriwa?

Je, hatuna sifa ya kuajiriwa?

Wadau tunaomba ushauri tujue nini cha kufanya.
 
Poleni. Mwl chichi aliwaambia mjiandae kisaikolojia.
 
ni hatari sana wahitimu wa ualimu katika chuo cha sekomu 2014 hakuna hata mmoja aliyepataajira sababu ya msingi etichuo hakitambuliwi kweli jamani TCU mpotupeni majibu ,tamisemi wanadai uongozi wachuo haukutuma majina ya wahitimu
 
Wakati wewe unahaha kuulza imekuwaje kutoonekana kwenye ajira, wenzenu wanalia na kuhaha kwa nini wamepelekwa vijijini, yaani mtu alitarajia anatoka (mfano) Tanga alafu apelekwe Dar, Arusha au Mwanza, Mbeya mjini, kumbe uhaba wa walimu ni vijijini siyo mijini.
Nawaomba vijana wangu mliobahatika kupata nafasi hizo nendeni kwanza mkaangalie opportunities za huko ulipopangiwa ndipo uone faida na hasara kwa eneo husika.

Naona kwenye ofisi za baraza na ofisi ya elimu walimu wapya wanajazana toka ijumaa iliyopita wakitaka kubadilishwa kutoka vituo vya shamba ili waletwe mijini, tena wengine wamebeba RUSHWA kuwapa maofisa ili wasipelekwe huko polini.
 
Supplementary wa mwaka jana hakuna hata mmojaa aliepata....dah..kaz ipo mtaani
 

Nimefanya tathmini ya haraka walimu waliopangwa Dar:

Walimu wa shule za msingi HAKUNA aliyepanvwa Dar!

Walimu wa sekondari stashahada na shahada masomo ya sanaa, HAKUNA aliyepangwa Dar!

Walimu wa sekondari stashahada na shahada masomo ya sayansi
Ilala 5
Temeke 4
Kinondon 16
 
Baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye ajira za ualimu zimetoka.?

Wadau tunaomba ushauri tujue nini cha kufanya.

Mkuu pole sana kwa jinsi tulivyokua tunasubiri ajira kwa hamu sipata picha jinsi mnavyoumia.

Ni kwamba situation kama hiyo ilitokea st John mwaka jana walimu wa BAED wote hawakupangiwa majina yalivyotoka kwa mara ya kwanza. Baadae ikaja kujulikana chuo kupitia department husika kilichelewesha kupeleka majina tamisemi.

Kwa hiyo chuo kilishughurikia hilo tatizo na baadae hata mwezi haukuisha watu wakapangiwa wote.

Kwa hiyo mimi niwatie moyo tu walimu wenzangu msikate tamaa matatizo kama haya hutokea. Kama chuo kipo makini kitashugurikia na mtapangiwa wote!
 
Hata hivyo post za sekondary zimetolewa zote na taarifa imewekwa pia jaribu kuwa na subira hadi zitakapo rudishwa tena
Na katika hilo tangazo wamezungumia hilo ulilo lieleza kuwa uongozi wa hicho chuo ulipeleka majina ya wahitimu wa mwaka 2013 badala ya 2014 hivyo wanarekebisha.
 

Nashukuru nimepata hiyo taarifa na tangazo hilo nimeliona. Hili hapa:
 

Attachments

  • 1430168616287.jpg
    36.9 KB · Views: 331
y

Chuo cha TEKU pia ngazi ya cheti hajaajiliwa mwl hata mmoja.
Diploma na Digrii wameajiliwa wote.
Hongeleni zenu kwa kuajiliwa.
 
y

Chuo cha TEKU pia ngazi ya cheti hajaajiliwa mwl hata mmoja.
Diploma na Digrii wameajiliwa wote.
Hongeleni zenu kwa kuajiliwa.

Chuo kimechukua hatua gan baada ya wanafunz wao kutoajiriwa? Sisi chuo chetu kipo active, mara tu ya kuona majina yetu hayapo walifanya mawasiliano ya haraka tamisemi na majina yote ymeondolewa
 
Subira yavuta kheri, ingawa hawajasema kama wale ambao tayari walishaona majina yao na halmashauri walizopangwa waende au wasiende. Hiyo ni dillema. Huenda ikaja list nyingine yenye halmashauri tofauti na ile uliyoona mwanzo. may b
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…