Mwaka wa ajira uliopita UDOM walituita kwenye interview. Hawakuchagua wenye sifa. Walituita watu wote tulioomba kazi. Matokeo yake kada moja ya nafasi 4 tulijikuta watu zaidi ya 5,000 tulienda kwenye interview. Pamoja na hayo, walitufanyisha interview ya kuandika kwa madai kuwa watakaofaulu wangewaita kwa interview ya pili ya kuongea. Cha ajabu waliwaita watu waliowataka wao tena kimya kimya bila kutangaza popote. Sisi wengineo bado tunasubiri hadi leo na tumesikia wenzetu wameshaitwa kazini. Sasa kwanini walituita wengi vile? kwanini hawakuchagua wenye sifa tu? Haya tuseme kwani wao hawafuati sheria ya serikali ya kupitishia ajira kwenye sekretarieti ya ajira? Serikali iwabane wapitishie ajira zao huko bwana waache kutusumbua. Utaratibu wa ajira zinatangazwa, watu wanaomba na wenye sifa wanaitwa kwa interview na kisha wanaitwa kazini. Hatua zote hzo zinatangazwa katika vyombo vya habari. Kwanini wao wasifanye hivyo? Serikali iwamulike kazi kwanza zitangazwe kupitia sekretarieti ya ajira kuepuka upendeleo kama huo. Waache mtindo wao huo. Na mwaka huu tena wakituita twataka posho ya nauli sie.