Ajira za utendaji wa mtaa/vijiji, ni kweli Tanzania inathamini elimu?

Na shahada yako wakupe 390K utawezana?

Kwanza now days hawachukui astashahada( cheti) wanachukua level 5 ambayo ni diploma 1.

Kama una wito na kuwa VEO/ MEO chukua vyeti vyako vya secondary ukasome., ganda lako la bachelor weka kabatini.
Sasa hivi kuna vijana wengi sana ni VEO/WEO.

Na hawa watu wana akazi nyingi sana zinazohusisha watu kila siku.

Bila VEO/WEO kazi za DEDs haziendi.

Ila sasa vijiji na kata nyingi ni porini mnooo ndio maana kazi hizi zinahitaji WITO.

Otherwise unaweza kuajiriwa kila siku ukawa unalalamika unaishi porini, hakuna nyumba na mshahara ni mdogo.
 
Basi wewe jiongoze wewe uwe tajiri wa mfano kuliko kusubiri ukaongoze kijiji kitajirike.
Yeye mmoja kashindwa kujiongoza anabaki kulalama tu! Akiongezewa malalamiko ya wananchi?
 
Nani kakudanganya kuwa mwenye astahahada sio msomi? Nani kakudanganya mwenye shahada ndio msomi?
 
Mkuu nakibalia na wewe. Enzi za Mwalimu tuliona wenye digrii (BA) wakiajiriwa mameja wa Vijiji. Leo wapo wengi wenye digrii hizo kwa nini wasijiriwe? Kama tumekubaliana miradi ya maendeleo iibuliwe kuanzia Vijijini, maana wao (wanakijiji ndio wanaojua vipaumbele vya miradi yao) kwa nini tusiwajiri vijana hawa? Au utaratibu huu haupo tena?
 
Tunaangalia kupewa kipaumbele elimu
 
Wekeni kwa kiingereza shahada,astashahada,uzamivu,uzamili wengine hawajui.
 
tatizo wasomi ukiwapeleka wakawe watendaji wa kijiji nanjiringi huko ndanindani hawataa wadumu huko wanatafuta uhamisho warudi mteni wasomi wengi wa tz bado tunakasumba ya kuamini kama umeshasoma basi unapaswa ukae sehemu nzuri kazi nzuri mjini na n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…