Ajira za walimu, awamu ya pili

Kkimondoa

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2014
Posts
4,453
Reaction score
4,933
SERIKALI itaajiri walimu wengine wapya wapatao 2,219, kufundisha katika shule za msingi na sekondari nchini. Walimu hao ni mbali na wengine wapya 33,894, ambao wameajiriwa hadi kufikia Mei 30, mwaka huu, Bunge lilielezwa mjini hapa jana.Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Elimu), Kassim Majaliwa alisema kwa mwaka huu wa fedha, serikali imeajiri walimu zaidi ya 36,000, ambapo walioripoti hadi Mei mwaka huu ni hao 33,894, hivyo kuacha pengo hilo la walimu 2,219. "Pengo hilo sasa litazibwa kwa kutangaza upya nafasi hizo.Tutatoa matangazo hayo katika mtandao wa Wizara hivi karibuni.

Nawaomba vijana waliohitimu vyuoni wafuatilie matangazo yetu hayo" alisema.Majaliwa alikuwa akijibu maswali ya msingi na nyongeza ya Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso (CCM). Alisema vijana wengi waliohitimu vyuoni, wamekuwa wakiiandikia wizara hiyo, kuulizia kuhusu ajira za ualimu.Aliwajulisha wahitimu hao kuwa wanaotakiwa kuomba kazi ya ualimu, lazima wawe wale waliosomea masomo ya ualimu katika ngazi ya vyuo vya ualimu au vyuo vikuu ;na siyo vinginevyo.Kwa mfano, alisema vijana waliohitimu Digrii ya Elimu katika Saikolojia au Digrii ya Elimu katika Utawala, hawawezi kwenda kufundisha sekondari, bali watapelekwa makao makuu ya wizara ya elimu kupangiwa kazi zingine.

Aidha, alisema vijana wengine waliohitimu Digrii ya Sheria na wana diploma ya uzamili wa sheria, au wamesomea fani nyingine, hawawezi kuajiriwa kama walimu, kwa sababu kimsingi hawajasoma masomo ya ualimu. Alisema watu kama hao , watafute kazi zingine, waache kuomba ajira za ualimu. Majaliwa alisema serikali imeanza kutatua tatizo la uchakavu wa miundombinu katika shule za msingi na sekondari na imeanza kupeleka fedha katika wilaya nchini, kukarabati miundombinu. Alisema tayari serikali imeshapeleka Sh milioni 50 kwa kila shule kongwe ya sekondari nchini kukarabati miundombinu.

Alisema serikali inaendelea kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Mpanda, kuboresha miundombinu ya shule ya msingi Kabungu ili ilingane na mazingira ya sasa.Katika swali lake la msingi, Kakoso alihoji "Shule ya msingi Kabungu ni ya muda mrefu toka enzi za mkoloni na majengo yake ni chakavu. Je, serikali iko tayari kujenga shule hii ili iendane na mazingira ya sasa?
 
inatia moyo kuona hivi ila tatizo huenda ikawa ni siasa tu ila ngoja tusubir
 

Mkuu taarifa kama hii inatia matumaini kwa wahanga
 
Je, kwa wale walio hitimu mafunzo ya ualimu mwaka huu 2014 watapata ajira mwaka huu?
 
jaman naomba kama kuna mpya zozote mnijuze kuhusu ajira hz za tamisemi,plz nd plz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…