Ajira za Walimu kutangazwa leo.

Ndala ndefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Posts
237
Reaction score
42
Ndg wapenda salam: Kutokana na taarifa nyeti nilizonazo ni kuwa ajira za Waalimu katika ngazi zote, yaani kuanzia ngazi ya cheti, diploma mpk degree leo zitatangazwa mda wowote kuanzia sasa na naibu waziri wa elimu ndg Mulugo. Asanteni na siku njema kwenu!
 
Itakua vizuri kwani watu wamesubiri hadi kukata tamaa.AHSANTE KWA TAARIFA KAMA NI KWELI....!!
 
Itakuwa poa sana mkuu, pia asante kwa kutoa taarifa ya kutia moyo. Mungu akubariki na kukutia nguvu.
 
kuna ukweli wa hili mkuu from 0657846028 maana tumekuwa tukiwadanganya na kuwachoha walimu wetu je kweli motisha ipo
 
Mwaka jana walitangaza 19/01/2012 mwaka juz n 26/01/2011 nadhan kwa range hyo mwaka huu watatangaza tarehe hizohizo au kati ya tarehe hzo.Walimu msikate tamaa mlikotoka ni mbali kuliko mnakoelekea.
 
mi nadhani serikali iwalipe pesa za kujikimu walimu hawa zote maana wajiandae kuzungushwa katika halmashauri watazopangwa maana kilio kikubwa ni kwanini serikali haitaji kiwango cha pesa za kujikimu watakazopewa walimu hawa.
 
walimu wote kupangwa vijijini sawa je wamewaandaje kukabiliana na mazingira hayo? wakati umefika tutumie ubongo wetu katika kutafakari hili maaana haiwezekani mwalimu anapangwa katika shule ambayo haina vitabu hakuna nyumba za walimu,huduma za kibenki zipo mbali,natumai post hizi zitaleta changamoto kubwa sana tusubiri
 
Bado tu hawajatangaza?mbona wanatuboa sana...wanafanya ufisadi gani hadi iwe ina suasua?
 

tunashukuru kwa taarifa,lakini siku ndio hiyo ishapita labda kesho au kesho kutwa si unajua hawaeleweki
 
Zikiwekwa naomba atakeziona anisaidie kunitumia sms kwa namba hii 0763631449 samahanini kwa hilo,vp kwa wizara ya afya nayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…