Mchoropa
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 402
- 304
IFIKE mahala siasa kama taaluma iwe na mipaka yake. Haiwezekani kuingiza siasa mpaka kwenye masuala nyeti ambayo ndiyo dira ya TAIFA! Hivi viongozi wetu ktk serikali mnawaza nini kuhusu ajira mpya za walimu??? mmetoa ahadi nyingi ambazo walimu wamekua na imani nazo na kuwataka wawe na subira, leo ni tar 15 ambayo ndiyo tarehe iliyosubiriwa kwa hamu sana na walimu ambao bado wapo mitaani kutokana na utaratibu wenu mbovu wa kuwaajiri, jambo la kusikitisha na kuvunja mioyo ya walimu hawa mpaka sasa bado hakuna taarifa rasmi ni muda gani mtaweka orodha ya majina ya walimu wapya walioajiriwa kama mlivyoahidi na kujinasibu, huku ni kuwakaribishia vidonda vya tumbo walimu wa watu@ IKO WAPI HIYO SERIKALI SIKIVU???