Huwa naingia majukwaa mbalimbali yanayotangaza ajira nadhani mara nyingi huwa naona kama changa la macho hakuna ukweli wowote juu ya uwepo wa ajira zilizotangazwa. Ikitokea kama kweli zipo basi kuna watu wameshapata hizo nafasi, na sie wengine tunaona machapisho tu mtandaoni lakini wenye kazi zao wapo, wanajua kila kitu na hata uwe na CV nzuri vipi, Cover Letter yenye ushawishi mkubwa huwezi pata kazi sababu hata kusoma barua yako hawatasoma.
Wakati mwingine unakuta kazi inahitaji mtu mwenye masters/PhD na experience ya miaka kumi katika field fulani ambayo kimsingi tangazo linakua specific sana mtu ukisoma kabisa unajua wanamtaka fulani mtu mmoja wanamjua job description wamecopy paste job experience yake.
Nadhani njia kabisa rahisi ya kupata kazi ni kwa kampuni kubwa ambazo huchukua wanafunzi waliotoka kuhitimu hapohapo ukikosa kazi hapo, basi jitolee bila malipo katika NGO , Kampuni binafsi, au katika taasisi ya serikali. Iwapo ajira zitatangazwa katika mahali hapo ulipo hata iweje wewe huwezi kukosa labda uwe na utovu wa nidhamu kipindi unajitolea, ila ukiwa katika ofisi watakavo tangaza ajira moja kwa moja utaipata sababu unajua miiko na maadili ya kazi, utendaji kazi ulivo nk. Kazi hizi zingine ndugu yangu utatuma maombi mpaka uchoke. Hadi naandika uzi huu nimeshatuma maombi zaidi 124 katika taluma zote nilizoona nafit na nimewahi pata email mbili tu za kuitwa kwenye interview na japo niliitwa kwenye kazi hizo zote zilikua ni part time na mkataba wa miezi sita. Email nyingine zote ni vya mbavu
Sidhani kama utaritibu inabidi uwe hivi kwamba lazima ufanye kazi bure ili upate ajira. Wengine kumudu maisha ya mjini(ambapo ajira zipo) ni changamoto na kushinda masaa nane kwa mtu bila malipo sio jambo dogo.
Natambua kampuni nyingi hasa kampuni binafsi, taasi za serikali, NGOs, na mashirika ya kitaifa na kimataifa, kwa mtiririko huo zinawatu katika idadi kubwa tu ambao uwezo wao sio madhubuti kuliko watu wanaokosa nafasi hizo nawezekana nisiwe mmoja wao, ila wapo watu wazuri, wenye vipaji, wenye akili lakini kazi hawana.
Je observation yangu hii si sawa?