Akadi, genius aliyeubadilisha mfumo wa elimu Tanzania

Akadi, genius aliyeubadilisha mfumo wa elimu Tanzania

Mulokozi GG

Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
34
Reaction score
44
Katikati ya kipindi ambacho ukosefu wa ajira ulikuwa wimbo uliozoeleka na ulioumiza sana kwa kila aliye kuwa na uwezo wa kuona vijana walivyo kuwa wanazidi kukosa mwelekeo ndani ya Taifa la Tanzania. Hatua ambayo wale wenye moyo wa kuhudumu wengine na walio majasiri pekee ndo wangeweza kusaidia.

Akadi Mtanzania aliyekuwa si maarufu kwenye masikio ya wengi, aliguswa sana na hali ilivyo kuwa inazidi kuwa tete kwa vijana na hakukubaliana na baadhi ya taratibu kwenye jamii hasa hasa zile ambazo matokeo yake yalikuwa hasi na ya muda mrefu kiasi cha kujengeka kama utaratibu au utamaduni. Kutokana na dhamira yake ya dhati kuwasaidia vijana na jamii nzima ya Watanzania, Akadi alianzisha chuo/kituo alicho kusudia kukiendesha kama kituo cha mafunzo kwa vitendo.

Mwanzoni kituo kilikuwa kinapokea wanafunzi walio tayari tu na kwa hiyari yao mwenyewe, msingi ukiwa ni uwezo wa kusoma na kuandika. Hivyo wahitimu kuanzia kidato cha nne hadi Chuo kikuu wote walipokelewa.

Mda wa kujiunga kila mwanafunzi aliye jiunga katika kituo hicho ilikuwa lazima awe na kitu kimoja maalumu alicho taka kujifunza katika nyanja anayo ipenda. Lengo kuu maalumu la kila mwanafunzi ndilo ilikuwa kama namba yake ya usajili. Kubadilisha lengo(specification) kilikuwa ni kigezo tosha cha mwanafunzi kuondolewa katika mafunzo au kupewa mda wa kutafakari uamuzi wake.

Mda wa mafunzo kwa mwanafunzi hadi kuhitimu ulikuwa katika vipindi vitatu. Miezi sita ya kwanza wanafunzi walifundishwa kujitambua(self determination), hapa alitumia wanasaikolojia na wakufunzi walio bobea katika maswala ya tabia. Lengo kuu la kipindi hiki lilikuwa kumfunza na kumsaidia mwanafunzi ajitambue na aelewe uwezo alionao. Ni katika hatua hii elimu juu ya ujuzi mbalimbali kama jinsi ya kuwasiliana (negotiation), kujifunza jinsi ya kujifunza, matumizi sahihi ya fedha na elimu ya hisia(emotional intelligence) vilifundishwa kulingana na uchaguzi na Lengo kuu la mwanafunzi.

Baada ya miezi sita ya kwanza, kipindi cha pili cha mafunzo kilicho kuwa cha miezi mitatu wanafunzi walifundishwa jinsi ya kuandaa, kufanya, kuandika na kuwasilisha tafiti (research).

Kutokana na uwezo pamoja na umahili alioonesha mwanafunzi kwenye yale aliyo funzwa. Wanafunzi waliombewa mikopo kutoka serikalini na kwenye taasisi mbalimbali, walipewa mda wa miezi sita hadi miezi kumi na mbili (kulingana na nyanja waliyopo) kufanya na kuandika tafiti zao pamoja na kufanyia majaribioa baadhi ya vipengele ndani ya tafiti walizo fanya. Kila mwanafunzi alifanyia tafiti kile kitu alicho sajiliwa nacho tu na kuwa nacho kichwani mda wote tangu alipo jiunga mafunzoni.

Baada ya tafiti kukamilika zilikuwa zinakusanywa na kutumwa kwa watu mbalimbali kuzipitia(kuzisahihisha) na kutoa maoni yao. Tafiti zote zilikuwa zinatumwa kwa watu walio katika nyanja husika. Mfano tafiti za biashara zilitumwa kwa wafanya biashara, za kitabibu zilitumwa kwa watabibu, za kilimo zilitumwa kwa wakulima nguli n.k. Kwa maneno mengine wasahihishaji wa tafiti walikuwa ni wale walio fanikiwa katika nyanja au fani husika.

Ajabu kama ilivyo baadhi ya wasahihishaji baada ya kumaliza kupitia tafiti walikuwa wanaahidi na kutoa nafasi za kazi kwa walio fanya tafiti hizo. Japo asilimia kubwa ya wanafunzi hao walikataa nafasi/ajira hizo kutokana na ujasiri, uzoefu na ujuzi walio kwisha upata walikuwa tayari kujiajiri wenyewe.

Mfumo huu ulianza kutekelezwa na Mtanzania mmoja tu Akadi, serikali ilivyo gundua limekuwa kimbilio la wengi iliamua kuanza kuufadhili kwa kuwapa kipaumbele kwenye mikopo wanafunzi wa Akadi, kutoa maeneo kwa ajiri ya tafiti na ujenzi wa vituo maalumu; ilianza pia kuutumia katika baadhi ya shule zake.

Baada ya miaka michache Taifa zima lilikuwa linatumia mfumo wa Akadi katika elimu, kwa kuwatuma wanafunzi ndani na nje ya nchi kufanya tafiti na majaribio juu ya vitu wanavyo taka kufanyia kazi kwenye maisha yao.

Katika uhalisia Akadi alipanda mbegu hii Tanzania kwa nia ya kusaidia kizazi cha Watanzania na siyo kupata kipato kikubwa kupitia mfumo huo. Changamoto ya ajira haikuwa tena tatizo kubwa ndani ya Taifa la Tanzania, hali iliyo pelekea kuanza kulitabili kama Taifa litakalo kuwa na nguvu zaidi Afrika.

Hadi kuwa mhenga(kuzeeka), Taifa zima lilikuwa limejaa sanamu zake na aliitwa majina mbalimbali kama Baba wa pili wa Taifa(baada ya Julius K. Nyerere), aliye jitolea kunusuru fikra za kizazi cha Watanzania.

Katika simulizi hii ni njia inayo weza kutumiwa kuubadilisha mfumo wa elimu siyo tu inaweza kutumiwa na Akadi(jina lililotumika ndani ya simulizi) bali inaweza kutumiwa na kikundi cha watu au mtu yeyote mwenye dhamila ya dhati na mwenye uwezo wa kujenga picha ya vizazi kadhaa vijavyo mbele, jinsi vitakavyo kua na kuishi; hivyo akaanza kuandaa mazingira sahihi Leo.
Kwani ukweli ni kwamba Tanzania, Afrika na Duniani kote ukosefu wa ajira siyo tatizo, tatizo ni elimu na elimu siyo tatizo, tatizo ni aina ya elimu.

Leo hii vijana wote wasio na ajira mtaani wakiajiliwa na mfumo wa elimu usipo badilishwa, ukaendelea kutoa wahitimu zaidi ya elfu hamsini vyuo vikuu kila mwaka. Haita chukua hata awamu Moja ya uongozi wa Raisi(miaka mitano), tatizo la ajira litakuwa pale pale na likiwa na makali zaidi.

Tusiiaminishe jamii yetu kuwa kutoa ajira kutaondoa tatizo la ukosefu wa ajira. Tatizo lipo ndani ya akili, mitazamo na Imani wanazo jengewa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Ni jukumu letu sote kuweka mfumo wa elimu utakao wafanya wanafunzi kujua misingi ya maisha tunayo ishi, kujiamini(self determination) na kuwaondolea kabisa dhana ya kuajiliwa.

Kila atakaye ingia katika mfumo wa elimu awe anajua fika kuwa anatafuta ujuzi atakao utumia maishani mwake yeye kama yeye kwa manufaa ya jamii yake. Atakaye ajiriwa iwe ni matokeo na siyo lengo kuu la mfumo wa elimu kwa jamii nzima.
 
Great thinker pekee ndio watakuelewa mkuu big up
Ila Kwa serikali hii ya ma CCM sahau kabisa Yani hayajiongezagi zaidi ya kupiga posho na mishahara minono minono akili zote zimehamia tumboni!
 
Katikati ya kipindi ambacho ukosefu wa ajira ulikuwa wimbo uliozoeleka na ulioumiza sana kwa kila aliye kuwa na uwezo wa kuona vijana walivyo kuwa wanazidi kukosa mwelekeo ndani ya Taifa la Tanzania. Hatua ambayo wale wenye moyo wa kuhudumu wengine na walio majasiri pekee ndo wangeweza kusaidia.

Akadi Mtanzania aliyekuwa si maarufu kwenye masikio ya wengi, aliguswa sana na hali ilivyo kuwa inazidi kuwa tete kwa vijana na hakukubaliana na baadhi ya taratibu kwenye jamii hasa hasa zile ambazo matokeo yake yalikuwa hasi na ya muda mrefu kiasi cha kujengeka kama utaratibu au utamaduni. Kutokana na dhamira yake ya dhati kuwasaidia vijana na jamii nzima ya Watanzania, Akadi alianzisha Chuo/kituo alicho kusudia kukiendesha kama kituo cha mafunzo kwa vitendo.

Kituo kilikuwa kinapokea wanafunzi walio tayari tu na kwa hiyari yao mwenyewe, msingi ukiwa ni uwezo wa kusoma na kuandika. Hivyo wahitimu kuanzia kidato cha nne hadi Chuo kikuu wote walipokelewa.

Mda wa kujiunga kila mwanafunzi aliye jiunga katika kituo hicho ilikuwa lazima awe na kitu kimoja maalumu alicho taka kujifunza katika nyanja anayo ipenda. Lengo kuu maalumu la kila mwanafunzi ndilo ilikuwa kama namba yake ya usajili. Kubadilisha lengo(specification) kilikuwa ni kigezo tosha cha mwanafunzi kuondolewa katika mafunzo au kupewa mda wa kutafakari uamuzi wake.

Mda wa mafunzo kwa mwanafunzi hadi kuhitimu ulikuwa katika vipindi vitatu. Miezi sita ya kwanza wanafunzi walifundishwa kujitawala(self Masterly), hapa alitumia wanasaikolojia na wakufunzi walio bobea katika maswala ya tabia. Lengo kuu la kipindi hiki lilikuwa kumfunza na kumsaidia mwanafunzi atambue uwezo wake na aweze kujitawala. Ni katika hatua hii elimu juu ya ujuzi mbalimbali kama jinsi ya kuwasiliana (negotiation), kujifunza jinsi ya kujifunza, matumizi sahihi ya fedha na elimu ya hisia(emotional intelligence) vilifundishwa kulingana na uchaguzi na Lengo kuu la mwanafunzi.

Baada ya miezi sita ya kwanza, kipindi cha pili cha mafunzo kilicho kuwa cha miezi mitatu wanafunzi walifundishwa jinsi ya kuandaa, kufanya, kuandika na kuwasilisha tafiti (research).

Kutokana na uwezo pamoja na umahili alioonesha mwanafunzi kwenye yale aliyo funzwa. Wanafunzi waliombewa mikopo kutoka serikalini na kwenye taasisi mbalimbali, walipewa mda wa miezi sita hadi kumi na mbili (kulingana na nyanja waliyopo) kufanya na kuandika tafiti zao pamoja na kufanyia majaribioa baadhi ya vipengele ndani ya tafiti walizo fanya. Kila mwanafunzi alifanyia tafiti kile kitu alicho sajiliwa nacho tu na kuwa nacho kichwani mda wote tangu alipo jiunga mafunzoni.

Baada ya tafiti kukamilika zilikuwa zinakusanywa na kutumwa kwa watu mbalimbali kuzipitia(kusahihisha) na kutoa maoni yao. Tafiti zote zilikuwa zinatumwa kwa watu walio katika nyanja husika, Mfano tafiti za biashara zilitumwa kwa wafanya biashara, za kitabibu zilitumwa kwa watabibu, za kilimo zilitumwa kwa wakulima nguli n.k. Kwa maneno mengine wasahihishaji wa tafiti walikuwa ni wale walio fanikiwa katika nyanja/fani husika.

Ajabu kama ilivyo baadhi ya wasahihishaji baada ya kumaliza kupitia tafiti walikuwa wanaahidi na kutoa nafasi za kazi kwa walio fanya tafiti hizo. Japo asilimia kubwa ya wanafunzi hao walikataa nafasi/ajira hizo kutokana na ujasiri, uzoefu na ujuzi walio kwisha upata walikuwa tayari kujiajiri wenyewe.

Mfumo huu ulianza kutekelezwa na Mtanzania mmoja tu Akadi, serikali ilivyo gundua limekuwa kimbilio la wengi iliamua kuanza kuufadhili kwa kuwapa kipaumbele kwenye mikopo wanafunzi wa Akadi, kutoa maeneo kwa ajiri ya tafiti na ujenzi wa vituo maalumu; ilianza pia kuutumia katika baadhi ya shule zake.

Baada ya miaka michache Taifa zima lilikuwa linatumia mfumo wa Akadi katika elimu, kwa kuwatuma wanafunzi ndani na nje ya nchi kufanya tafiti na majaribio juu ya vitu wanavyo taka kufanyia kazi kwenye maisha yao.

Kwa ujumla Akadi alipanda mbegu hii Tanzania kwa nia ya kusaidia kizazi cha Watanzania na siyo kupata kipato kikubwa kupitia mfumo huo. Na changamoto ya ajira haikuwa tatizo kubwa tena ndani ya Taifa la Tanzania, hali iliyo pelekea kuanza kulitabili kama Taifa litakalo kuwa na nguvu zaidi Afrika.

Hadi kuwa mhenga(kuzeeka), Taifa zima lilikuwa limejaa sanamu zake na aliitwa majina mbalimbali kama Baba wa pili wa Taifa(hapa wakimaanisha baada ya Julius K. Nyerere). Mitaani walimuita Baba wakambo wa Taifa aliye jitolea kunusuru fikira za kizazi cha Watanzania baada ya mwalimu Nyerere kulipatia Uhuru Taifa hilo.

Katika simulizi hii ni njia inayo weza kutumiwa kuubadilisha mfumo wa elimu siyo tu inaweza kutumiwa na Akadi(jina lililotumika ndani ya simulizi) bali inaweza kutumiwa na kikundi cha watu au mtu yeyote mwenye dhamila ya dhati na mwenye uwezo wa kujenga picha ya vizazi kadhaa vijavyo mbele, jinsi vitakavyo kua na kuishi; hivyo akaanza kuandaa mazingira sahihi Leo.
Tanzania na Afrika ukosefu wa ajira siyo tatizo, tatizo ni elimu na elimu siyo tatizo, tatizo ni aina ya elimu.

Leo hii vijana wote wasio na ajira mtaani wakiajiliwa na mfumo wa elimu usipo badilishwa, ukaendelea kutoa wahitimu zaidi ya elfu hamsini vyuo vikuu kila mwaka. Haita chukua hata awamu Moja ya uongozi wa Raisi(miaka mitano), tatizo la ajira litakuwa pale pale na likiwa na makali zaidi.

Tusiiaminishe jamii yetu kuwa kutoa ajira kutaondoa tatizo la ukosefu wa ajira. Tatizo lipo ndani ya akili, mitazamo na Imani wanazo jengewa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Endapo mfumo wetu wa elimu hauta badilishwa ni dhahili mbeleni kuna vilio vingi zaidi.

Suluhisho la vilio hivi ni kuweka mfumo wa elimu utakao wafanya wanafunzi kujua misingi ya maisha tunayo ishi(self masterly), kujiamini na kuwaondolea kabisa dhana ya kuajiliwa.

Kila atakaye ingia katika mfumo wa elimu awe anajua fika kuwa anatafuta ujuzi atakao utumia maishani mwake yeye kama yeye kwa manufaa ya jamii yake. Atakaye ajiriwa yawe ni matokeo na siyo lengo kuu la elimu kwa jamii nzima.
 
Back
Top Bottom