Akanipandishia gauni ili nione vizuri…………………!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Mkasa huu ulinipata Mwaka 1999, nakumbuka nilikuwa katika kuhangaika kutafuta kibarua, nilijikuta nikiwa kwenye ofisi moja ya jamaa yake kaka. Nilifika hapo baada ya kaka yangu kuzungumza na huyo jamaa yale kuhusu ajira. Ilikuwa nikamwone ili kuona uwezekano wa kupewa ajira. Nilifika hapo ofisini kwa jamaa yake kaka kiasi cha saaa 2.15 asubuhi. nilipofika mapokezi, ambapo pia palikuwa panatumika kama ofisi ya watumishi wengine, nilikuta watu watano, wote wanawake. Mwanaume alikuwa mmoja, ambaye wakati naingia, naye alikuwa anatoka.

Nilisalimia na kumwambia katibu muhtasi shida yangu, ambapo aliniambia nikae kumsubiri bosi, ambaye kwa kawaida anafika pale ofisini saa tatu asubuhi au zaidi. Nilikaa kando kwenye makochi. mbele yangu kulikuwa na mwanamke ambaye alikuwa anafanya kazi zake. Alikuwa amekaa kihasara kwa kweli. Akiwa amevaa gauni fupi, alikuwa amaeachia mapaja yake wazi na niliweza hata kuona kule kunako utukufu bila wasiwasi. Nikiwa kijana shababi niliamua kufaidi sinema ile ya bure katika kupitisha muda kumsubiri bosi. Kwa hiyo nikawa napiga jicho kwenye mapaja yake ya haja maana mwanamke mwenyewe alikuwa ameumbika hasa. Nikiona yule dada ananitazama, navunja shingo na kujifanya simtazami yeye.

Niliendelea na sinema ile kama robo saa tu kabla yule dada hajaacha kufanya kazi yake. Alichukua kiti chake na kukitoa kutoka kwenye meza na kuja nacho karibu na makochi nilipokuwa nimekaa. Sikujua anafanya vile kwa sababu gani. Alipokiweka kiti kile pale mbele yangu, alipandisha gauni lake fupi hadi juu kabisa. Alipomaliza kufanya hivyo alikaa kitini huku akinitazama. Wale wanawake wengine pale ofisini waliacha kufanya kazi na kushikwa na mshangao. ‘Vipi mwenzetu, kuna nini kumekupata?' Mmoja kati yao alimuuliza yule dada. ‘Nataka ayatazame mapaja na vingine kwa karibu ili afaidi sana. Naona anapata shida kuibaiba, haya tazama baba uridhishe nafsi yako.'

Kila mmoja alielewa maana yake, nikiwemo mimi. Ni kweli, nilikuwa ninamtazama kwa hila, lakini haina maana kwamba, nilikuwa namchungulia. Nilibaki nimeduwaa, nimepigwa na butwaa kubwa sana. Mmoja kati ya wale wanawake alisema, ‘dada Glady naye haishi vituko, hebu mwache kijana wa watu...' mwingine alidakia, ‘utamweza Glady vituko vyake basi!' yule mwanamke ambaye sasa nilijua anaitwa Glady alisema, 'hapana, wanaume wengine bwana hawana adabu, macho wayuwayu sana. Nataka kiu yake iishe leo. Hebu cheki sasa uridhike.

Mlio wa gari la bosi wao ndiyo ambao uliniokoa kutoka katika kadhia ile. Aliposikia mlio huo wa gari, aliinua kiti chake na kurudi mezani pake huku akisema, ‘bahati yako, ungeniambia leo, nini kinang'aa zaidi, nyota au mbalamwezi.'
 
Nisije nikaona Cantalisa na King'asti wamechangia huu uzi, patachimbika..................!!!
 
Alikuwa sawa na msaada kwako. Pia fyatu kwelikweli, as if anapuliza!
 
Duh pole sana, ila ukute huyo dada Glady ndo tabia yake ndo mana hata wafanyakazi wenzake walisema haachi vituko.
 
Baby sister unataka begi jipya la shule? Ntakuambia tukitoka skuli
Shikamoo baba,mie wala sichangii kbs,ila nauliza eti baba baada ya pale nn kilitokea?kazi ulipata?leo wala ctakusemea kwa mama!hadithi hii inatufundisha nn baba?
 
Shikamoo baba,mie wala sichangii kbs,ila nauliza eti baba baada ya pale nn kilitokea?kazi ulipata?leo wala ctakusemea kwa mama!hadithi hii inatufundisha nn baba?

Marahaba Mwanangu. Kama unataka kumuona huyo Glady, ofisi anayofanya ipo hapo Victoria njia ya kwenda Mwenge, nashukuru kazi nilipata na amekuwa mfanyakazi mwenzangu na ni dada yangu wa hiyari.................

Simulizi hii inatufundisha tusiwe tunapiga CHABO kina dada wakikaa kihasara hasara, tutapofuka...............
 
Baby sister unataka begi jipya la shule? Ntakuambia tukitoka skuli
Nilikuwa nakuhofia wewe tangu mapema nandio sababu ya kuweka angalizo, lakini kwa jinsi ulivyombishi ushaanza mapemaaa......... Nimeshakuonya, patachimbika hapa.....OOhoooo!!!
 
Duh! kakufunulia kabisa anaona unapata shinda,hajui kama ndio raha yenyewe vikiwa tabu kuviona,au babu ulimkodolea sanaa machoo?
 
Brother-kaka, mtu anapoenda kutafuta kazi sehemu flani anakuwa na wenge sana. Sasa ukiongeza na hiyo show, nadhani uliloa hadi kucha.
 
sawa ili fundisho, lkn huyo dada glady ni balaa.................................mwambie nampa asalamalyek bi dada huyo mmh.
 
Baba, mbona huyu dada yako wa hiari sijawahi kumuona akija hm?
Mbona ww ulipiga chapo na unato macho yako mpaka sasa na hujapofuka?
Je ni ruhusa kpiga chabo akina kaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…