Akaunti gani ya NMB ni bora zaidi kwa kutunza hela?

Akaunti gani ya NMB ni bora zaidi kwa kutunza hela?

Graxsam

Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
83
Reaction score
94
Wadau nataka kufungua akaunti ya nmb bank kwaajili ya kutunza hela zangu je ni akaunti gani nzuri?
 
Nunua hisa Kama hauna kazi nayo recently
Yeye anataka kutunza hela, hisa zinaweza kushuka hivyo thamani yake ya pesa ikashuka, labda angejiunga na UTT Amis ambao pesa yake itaongezeka kwa 1% (approximately) per month au anunue hatifungani za benki kuu.
 
Kwa Nmb bonus account ni suluhisho la kutunza pesa zako bila umbea, haukatwi makato ya mwezi, kutoa kwa miezi mitatu una ruhusiwa kutoa mara 1 bila kuathiri riba yako ya bonus kutokana na kiwango ulicho weka kwenye account nawasilisha.
 
Kianzio ni Tsh ngapi
 
Wadau nataka kufungua akaunti ya nmb bank kwaajili ya kutunza hela zangu je ni akaunti gani nzuri ?

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Kwangu mimi naipenda hii banki kwa kutunza hela kwa sababu zifuatazo
1. Kila ukitaka kuweka saving ni rahisi sana
2. Wako vizuri sana kutoa taarifa kila utunzapo pesa
3. Inapatika kwa urahisi sana
Itumie kwa kutunza hela maana wabongo kutunza pesa sisi na mimi nikiwemo ni mtihani sana

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Kwa Nmb bonus account ni suluhisho la kutunza pesa zako bila umbea, haukatwi makato ya mwezi, kutoa kwa miezi mitatu una ruhusiwa kutoa mara 1 bila kuathiri riba yako ya bonus kutokana na kiwango ulicho weka kwenye account nawasilisha.

Hakika hapo umenena Na Mie ninayo ni mwaka sasa sijawahi ona wanakata zaidi wanakupa bonas tu [emoji392]
 
Ushauri wa kuzitunza pesa zako UTT (hasa mfuko wao wa liquid kwa lengo lako) ni mzuri - kuliko benki kwenye masharti kibao licha ya riba ndogo zaidi.
 
Back
Top Bottom