Akhsanteni sana Waandaji wa Ndondo Cup kwani nimeuza sana Bangi, Kuberi, Simu za Wizi na Gongo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nipende tu kuchukua fursa hii adhimu kuweza kuwashukuru sana na mno Waandaji wote wa Mashindano ya Mpira wa Kihuni / Kisela wa Ndondo Cup kwa kuweza kunifanya niweze kupata faida Kubwa ya Kuuza mule ndani Kinesi Stadium Bangi, Kuberi, Simu za Wizi na pombe ya Gongo hali iliyonifanya nichukie sana Mashindano hayo kuisha kwani sitokuwa na Soko tena hadi msimu ujao.

Nitoe tu ushauri kwa Waandaji wote wa Ndondo Cup kuwa kama mtaweza basi muwe mnayaandaa haya mashindano hata mara mbili ndani ya mwaka kutokana na kwamba Sisi wengine huwa tunapata Ajira za Uhakika za Kuuza Bangi, Kuberi, Simu za Wizi na Gongo katika Viwanja vyenu ila hasa hasa Biashara yangu hii hunoga mechi zinapokuwa Uwanja wa Kinesi kwakuwa ni karibu sana na kule ambako nimekuwa nimeweka stock yangu ya Kutukuka ya hivyo vitu.

Mwisho niwaombe tu Wadau humu kama mnajua Kiwanja kingine chochote ambacho naweza kwa sasa kwenda kuuza hizo bidhaa zangu adimu na muhimu hasa hapa Jijini Dar es Salaam tafadhalini hebu niambieni ni wapi ili nijipange na mchana niweze kwenda kwani hii Biashara inalipa kuliko hata Kusafirisha mchanga wa Makinikia.

Nawasilisha.
 
sitashangaa mods wakikurupuka na kukupiga ban bila kuelewa kilichomo kwenye mada yako
 
ndio biashara iliyopamba mashindano hayo,,okei
 
Umetumwa na DAB wewe

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app
 
Sio kweli mimeenda game nyingi kinesi watu walikua wanapiga picha na simu zao sijaona mtu alalamike kuibiwa . Halafu hata huko nje wametokea huku mwaka Tottenham wanafanya uwanja wao.

Fikilia wauza maji, karanga, machungwa na chakula wangapi walijiajiri kupitia ndondo cup ndio uje na lawama.

Bila kusahau wauza nazi aina ya mbaya, mihogo na karanga mbichi
 
Hakuna kitu positive ulichokiona kwenye Ndondo? Tuachieni wenyewe wa uswazi mambo yetu watoto wa Kota hamuyawez
 
Ukitaka kutoboa kwa njia hiyo, nakushauri amia katika wilaya ya Temeke.

Wezi na wahalifu kama wewe huku wako vizuri sana, Ndondo inapo fanyika katika viwanja vya Bandari, Walinzi wa kiraia ukiunganisha na Askari polisi, wote wanatokea Nyumbani Temeke, hivyo watu wanauziwa Bangi, Kubeli na hizo Gongo na Viroba kwa Uhuru na Uwazi....

Ukijisikia kutumia humo humo Uwanjani ni maamuzi yako..

Rudi sasa kwenye Mechi za Ligi (VPL) Mechi za Kimataifa...zile za kirafiki....!!

Viwanja vya Taifa na kile cha Chamanzi, ni sehemu za Mawindo na maeneo ya Vibaka hasa kutoka Temeke kutafutia Riziki na Mitaji ya kuendesha maisha yao...!!

Temeke...a nice en better place for Survival (hard working)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…