Wakuu wana wa JF na wenye taaluma ya afya, Salaam!
Nina mwanangu wa kiume wa miaka sita na anasoma shule ambayo humfanya tumwamshe kila siku ya shule saa 11:45 asubuhi.
Akiamka na kusimama kwenye sinki ili kupiga mswaki huwa analalamika miguu inachoka na hudai apige mswaki amekaa.
Swali langu je, huu huwa ni usingizi tu au ugonjwa fulani unajengeka?
Hali hii hutokea asubuhi tu anapotoka usingizini.