JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Imeelezwa kuwa uhitaji wa damu uliopo Nchini ni kati ya chupa laki tano na nusu mpaka sita huku akiba iliyopo ni chupa laki tatu na sabini na tano, hii ikiwa ni takwimu zilizofanywa mwaka 2021.
Hayo yamesemwa na wakati wa uchangiaji wa damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Damu inayofanyika kila mwaka Juni 14.
Afisa Mhamasishaji Jamii Damu Salama Kanda Mashariki, Mariam Juma amesema ni muhimu kwa jamii kujitoa katika kuchangia damu kwani uhitaji bado ni mkubwa.
"Jamii inahitaji kujitolea damu maana wahitaji ni wengi na huwezi jua leo kwa mwenzio kesho kwako," anasema Mariam.
Amewataka wananchi kutokuamini dhana potofu kwamba ukitoa damu ndio chanzo cha kulazimika kutoa damu mara kwa mara.
Naye Meneja Mkuu wa Assembly Insurance, Tabia Masoud amesema wao wameamua kujitoa kufanya kazi hiyo Juni 17 kutokana na kuona umuhimu wa kuchangia damu inayohitajika.
Alisema wao ni taasisi ya Bima wanazunguka na kuona kwamba uhitaji wa damu na hata kwa wateja wao ni mkubwa hivyo wametumia siku ya leo katika kuchangia damu.