Akiba ya Dhahabu G.O.T

Akiba ya Dhahabu G.O.T

Mbegu Jr

Senior Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
152
Reaction score
178
Yanaoendelea ndani ya Dunia yetu Kwa nyakati hizi za sasa

Hapo nyuma kidogo kulikuwa na COVID-19,Kwa Sasa tuna vita vya Ukraine.

Haya matukio Kwa taarifa zinazotolewa inaonesha ni Kwa nanma Gani hakuna kitu Cha bahati mbaya.
Sisi watanzania tunacho Cha kujifunza na kuchukua hatua kutokana na hali kama hiyo.

Akiba yetu ya fedha za kigeni isiwe ndio kitu pekee Cha muhimu tunacho takiwa kuwa nacho Kwa kiwango kikubwa.

Mataifa mengi Sasa hivi yameanza kujiondoa kutoka kutumia Dollar kama means of transaction,ilianza Kwa china na Rusia Sasa inaelekea Kwa BRICS wote hata sisi Tanzania tumeingia makubaliano na India tufanye biashara Kwa currency zetu na sio kama ilivyo zoeleka,naomba niishie hapa niende kwenye lengo mama.

Serikali yangu ningeshauri iongeze manunuzi ya Dhahabu ili kuwa na kiwango kikubwa kuliko hapo miaka ya nyuma uzuri ni kwamba madini haya tunayo ndani ya taifa letu.

Tishio la Vita ya tatu ya Dunia ni kubwa Kwa Sasa hivi.

Hii inaweza kuwa msaada Kwa taifa bila kujali madhara yatakayosababishwa labda tufe wote
Ila hata wakibaki watu kumi kwenye taifa kuwepo na AKIBA KUBWA YA DHAHABU. Kuanzia Sasa hivi na kuendelea
Ikiwezekana wizara ya Mipango ifanye hii ni Moja kati ya ajenda kwenye dira inayoanza kuandaliwa ya miaka 25 ijayo na kuendelea.

Pesa ya MAREKANI inawezekana isiwe tena reserve kama ilivyo Sasa Kwa miaka ya baadaye lakini Dhahabu itakuwa akiba Kwa vipindi vyote na Kuna uwezekano mkubwa WA Gold kuendelea kupanda thamani huko mbele.

Reserve Much Gold.
 
Back
Top Bottom