Msemo huu kwa sasa umekuwa maarufu sana katika mtandao huu, na wengi huutumia kutoa tahadhari kwa mtu/watu anayetumia maneno yote kumshtumu mtu/watu fulani kudhihirisha kuwa mtu/watu huyo/hao hafai/hawafai kabisa.
Mathalani siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la watumiaji wa JF kufukua nyuzi za zamani ambazo zilikuwa zikimshutumu Lowassa wakati akiwa CCM kwa matusi kemkem, na kwa sasa wanatumia kila aina ya mbinu kumtetea.
Hawa hawakuwa na akiba ya maneno.
Je ni nani aliupa umaarufu msemo huu?
Usidanganye.......anajulikana.
NB: Changia kwa ustaarabu TCRA wapo kazini, waulize clouds ama ITV