WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Kuna kipindi cha radio kinazungumzia mada ya mahusiano baina ya wanawake na wanaume.Kitu kilichonistua ni ujumbe uliosema " akikutaa kimapenzi basi na urafiki ufe".Ina maana wanawake na wanaume hakuna urafiki isipokuwa mapenzi? Inakuwaje kwa wale ambao hawana " uwezo" wa kutoa penzi ?
...WOS,....mijitu ya aina hiyo haina tofauti na wale waajiri wanaogomea ajira mpaka wapewe penzi!
Sijui haina ndugu wa kike kwao?
Mwenzio akikataa kuwa mwenzi wako kimapenzi....usilazimisha. Unaweza endelea na urafiki kama kawa. Tena kwa uzoefu wangu mimi ndiyo una-kuwa free nae sana!:violin:Kuna kipindi cha radio kinazungumzia mada ya mahusiano baina ya wanawake na wanaume.Kitu kilichonistua ni ujumbe uliosema " akikutaa kimapenzi basi na urafiki ufe".Ina maana wanawake na wanaume hakuna urafiki isipokuwa mapenzi? Inakuwaje kwa wale ambao hawana " uwezo" wa kutoa penzi ?
Urafiki gani tene utakuwepo hapo, marafiki hushare intrst, na intrst yako wewe ni kugongana, na yeye hataki kugongana....PIGA CHINI.
kwahiyo huo urafiki wa maslahi ila ule urafiki wa kweli kabisa hauwezekani!!!! labda awe gay!!!!Kwa kweli nimeshtuka..nikakumbuka kwenye mashule kuna wasichana na wavulana huwa na urafiki wa kushirikishana mambo ya masomo, nikaingia maofisini nikajiuliza inakuwaje kwa workmates ambao hujikuta wakielewana sana kwa sababu ya mambo ya kazi.Nikaja sehemu za biashara ambapo wanawake na wanaume huweza kuwa na networks ambazo hazihusu " mapenzi"... nikajikuta najiuliza maswali mengi.Ina maana wanaume hawa wote wanalenga kupata penzi? Jibu likaja kuwa " siyo lazima...."
Kama ulivyosema, watu kama hawa waweza kusababisha tafrani kwenye jamii!!...
Lakini kabla hatujamhukumu...... huenda kuna ujumbe anaotaka kuutoa, labda hatujampata vizuri?
Hao watakuwa na matatizo kwa hiyo yeye kila akiwa na rafiki wa kike lazima atoe penzi ? inatisha