Akila chakula anapata maumivu kifuani usawa wa kwenye moyo na pumzi inakata. Inaweza kuwa ni shida gani hii?

Asante sana mkuu, nadhani amekupata vizuri.

Binafsi nilibadili tu mfumo wa ulaji na nimekaa sawa kiasi fulani
 
Ndugu Taitu2024 wakati mkiendelea kutafuta matibabu jaribuni kuzingatia haya

1. Lishe Bora:
- Epuka vyakula vyenye asidi nyingi: kama matunda ya machungwa, nyanya, na vyakula vya pilipili.
- Epuka vyakula vyenye mafuta mengi: kama vile vileo, chips, na chakula cha kukaanga.
- Kula chakula kidogo mara kwa mara: badala ya kula milo mikubwa.
- Usile karibu na wakati wa kulala: jaribu kula angalau masaa mawili hadi matatu kabla ya kulala.

2. Mabadiliko ya Maisha:
- Punguza uzito: ikiwa una uzito wa ziada, kupunguza kilo kadhaa kunaweza kusaidia.
- Va nguo zisizobana: nguo zinazobana zinaweza kuongeza shinikizo kwenye tumbo.
- Inua kichwa wakati wa kulala: tumia mto kukuboresha kichwa chako chote zaidi kutoka usawa wa kitanda.
- Epuka kuvuta sigara: sigara inaweza kuzidisha reflux.

3. Vinywaji:
- Epuka kafeini na pombe: vinaweza kuongeza dalili za GERD.
- Kunywa maji mengi: maji yanaweza kusaidia kupunguza asidi ya tumbo.

4. Dawa:
- Antacids: hizi ni dawa ambazo zinaweza kupunguza asidi ya tumbo.
- H2 Blockers na Proton Pump Inhibitors (PPIs): hizi ni dawa zinazosaidia kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni. Fahamisha daktari wako ili kupata ushauri bora kuhusu matumizi yake.

5. Mazoezi:
- Fanya mazoezi mara kwa mara: lakini usifanye mazoezi mazito baada ya kula.
- Mazoezi mepesi: kama vile kutembea inaweza kusaidia usagaji chakula.

6. Usimame na Kulala Vizuri:
- Usilale baada ya kula: subiri masaa kadhaa baada ya kula kabla ya kulala.
- Simama wima baada ya kula: kunyanyuka wima na kutembea inaweza kusaidia kuzui reflux.

7. Punguza Stress:
- Fanya mazoezi ya kupumzika: kama yoga na meditation.
 
Poleni sana. Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi mgonjwa.
 
Azingatie haya atapona, mimi ni shuhuda nilishapitia Hilo tatizo, chanzo kikuu inaweza kuwa msongo wa mawazo.
 
Huyo mtu ana kitu kinaitwa acid reflux

1. Asile chakula kingi usiku na ale mapema asubiri kama lisaa ndio alale

2.asitumie maharage,vitu vichachu,pili pili aache kabisa

3.aepuke msongo wa mawazo
 
Wamesema ni sonona
Kama ni sonona, kuna mawazo mazuri sana yametolewa hapo juu. Suala la kudhurika kwa njia ya chakula linabaki wa sehemu ya shida kwa sababu tajwa.

Kwani kulingana na kiasi cha sonona na muda na muunganiko wa haya huweza kutokea:
1: aina ya lishe anayokula isiwe njema
2: kiasi cha lisha kisiwe cha kutosha
3: hamu ya chakula kutokua nzuri
3: uzito wake kupungua
4: mfumo wa kinga kuteteleka
5: vinywaji wakati wa sonona
nk.

Kwa sababu hatuwezi kufahamu kiasi cha tatizo ni vyema tiba yake kusimamiwa na:

1: Mwanasaikolojia au daktari wa afya ya akili kulingana na chanzo pamoja na kiasi cha tatizo. Hawa watamsaidia kwa upande huo wa utimamu wa afya yake ya akili.

2: Daktari bingwa wa njia ya chakula/Gastroenterogist: hii itasaidia kujua kiasi cha tatizo na jinsi ya kulikabili, uhitaji wa vipimo zaidi au la.

Hii itatoa wholistic management/tiba jumuishi badala ya tiba ya kimoja kimoja.

Kwani sonona yaweza kuwa ni sababu ambayo imepelekea shida nyingine/gastritis. Ukitibu kimoja peke yake hautapata mwendelezo/ matokeo mazuri na inaweza kuwakatisha tamaa mgonjwa na wauguzaji. Kumbe shida ni kushughulika na kimoja na kuacha kingine nyuma.

Hivyo, tiba ya saikolojia, lishe, dawa na mabadiliko kwenye mwenendo wa maisha utakuwa ni msingi wa matibabu yake.

Tiba njema na poleni sana.
 
Asante I sana wadau Kwa ushauri wenu ni kweli tatizo la msongo wa mawazo ndo wamesisitiza Hana shida nyingine lkn shida ya huo mfumo wa chakula imetokana na msongo wa mawazo lkn madakitari wamesisitiza tatizo Moja tu la msongo wa mawazo na naona hili la chakula litaleta madhara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…