Akili hasi kamwe haiwezi kutoa matokeo Chanya

Akili hasi kamwe haiwezi kutoa matokeo Chanya

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Hii ni kwa wale watu wabishi wabishi hata kwenye Jambo la msingi yeye anataka kukwamisha. Unakuta mtu kafanya jambo lake analifurahia atatokea mtu tu kuhakikisha anakuliza.

Hawa watu tunaishi nao Kazini,nyumbani, Shuleni kwenye Biashara. Hakikisha unawakwepa au unawazoea watu kama hao.

Unakuta unataka kujaribu kufanya kitu mtu anakwambia walishindwa sijui kina nani wewe utaweza?
Na wewe unaamini, unaacha kufanya.

Ndugu yangu hapo ndio unawafanya wafurahi sasa wamekukwamisha. Ukiamua kufanya kitu fanya tu bila kujali ushauri wao ili mradi kiwe chenye tija na usjvunje Sheria za nchi.
 
Back
Top Bottom