Mtazamo wangu baada ya kuwatazama Barcelona dhidi ya Madrid, nimegundua kwamba, pamoja na kufanya mazoezi ili mchezaji aweze kucheza soccer kikamilifu na kung'ara anatakiwa pia awe na akili kubwa.
Akili kubwa itamfanya mchezaji kufuata maelekezo ya kocha akiwa kwenye mechi na pia itamuwezesha kutafsiri matukio kwa haraka mfano kupiga chenga, kutoa pasi nk. Hapa ndipo utasiki kocha anasema hawa wachezaji wanafundishika, lakini wale hawafundishiki.
Kwa mfano, Barcelona ina wachezaji vijana wenye akili kubwa ndiyo maana waliweza kuwa-win wachezaji wa Madrid.
Mfano mwingine, wale mabeki wa Barcelona walifanikiwa kucheza offside triki na wachezaji wa Madrid wakaotea zaidi ya mara tano. Hii ni akili kubwa kwamba wanakuwa wapo mchezoni muda wote na kufuata maelekezo ya kocha. Kungekuwa na akili ndogo kwenye ile beki ya Barcelona lazima mmojawapo angechomesha.
Mchezaji mwenye akili ndogo anashindwa kutafsiri matukio kwa haraka akiwa uwanjani. Sehemu ya kutoa pasi ili mwingine afunge, hafanyi hivyo bali analazimisha afunge yeye na anakosa.
Hivyo, tujitahidi kuwajengea watoto mazingira ya kuwa na akili kubwa kwa sababu hata katika vipaji akili kubwa inahitajika pia mfano katika soccer, utunzi wa muziki nk.
Akili kubwa ya mtoto itaanza kujengwa tangu siku ya kutungwa mimba ambapo mama mjamzito anatakiwa afuate ushauri wa daktari katika masuala ya lishe. Pia. mtoto akizaliwa anatakiwa apewe lishe bora