MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Kwa mara ya pili, rais Uhuru amealikwa kwenye kikao cha G7 ambacho ni mkusanyiko wa mataifa machache yenye ushawishi mkubwa duniani, na kualikwa humo uhutubie na kueleza lazima uwe umekaguliwa uwezo wako, michango yako na ushawishi wako kwenye ukanda unaotokea.
Ikumbukwe Kenya mwaka jana ilikua mwenyeji wa wageni 18,000 waliotokea kwenye mataifa 170 duniani ambao walikuja kuhudhuria kikao cha kwanza kuwahi kutokea duniani cha kujadili uchumi wa bahari, maziwa, mito na maeneo yote yenye maji (blue economy).
Huo hapo ni mfano mmoja tu wa jinsi gani Kenya chini ya uongozi wa rais Uhuru, imechukua nafasi ya kuiongoza Afrika kwenye kila hali, na zaidi ya yote Kenya leo hii ndio inaongoza kiuchumi, kijeshi, kielimu ukanda wote huu, imeipiku hata Ethiopia, yaani kote hadi hata Afrika ya kati.
Ni fahari kwa rais wetu kualikwa kwenye vikao kama hivi, maana kwa wanaoelewa siasa za kimataifa na diplomasia wanajua ni jinsi gani taifa hufaidi linapopigiwa debe kihivi, na humo kama ilivyo kawaida yake rais, atakua na vikao vya faraghani pembeni na kila rais wa hayo mataifa ambayo ndio huongoza dunia na kuelekeza sera.
Hii hapa video anavyotema yai kuhusu sera za kutambua mchango wa wanawake kwenye uongozi....hamna cha zezeze