bartenderznz
JF-Expert Member
- Jul 18, 2016
- 398
- 195
Jana nilikaa na mwanangu wa miaka 4 na ushei hivi,nilizungumza na kucheka nae kitoto,niligundua anajua mambo mengi ya ulimwengu huu wa digitali,likanijia wazo la kumuhamisha chumbani kwangu ili alale pakee yake.
Nilimueleza kuwa amekuwa mkubwa na anatakiwa alale peke yake .Nilimueleza kuwa amekuwa mkubwa hapaswi kulala pamoja na baba na mama.Nilimueleza mambo mengi yanayohusiana na ajenda yangu.
Baada ya maelezo yote hayo niliyomueleza kwa upole.Nilipigwa na butwaa pale aliponiuliza "Mbona wewe dady ushakuwa mkubwa na unalala na mama"?
Sent using Jamii Forums mobile app