Utangulizi;
Jambo linalo mtofautisha kwa kiasi kikubwa binadamu na viumbe wengine ulimwenguni ni akili (sina maana ya ufaulu darasani maana mfumo wetu wa elimu umeshindwa kubainisha utofauti wa viwango vya akili mashuleni kupitia mitihani pekee kwani ufaulu wa juu sio pekee ndio kipimo cha akili) ingawa wengi huhusanisha akili nyingi na kipaji au kipawa.
Wengi wanaposikia nguvu akilini mwao inajengeka picha ya jasho jingi , misuli na uchovu pekee, la hasha unaweza pia tumia nguvu nyingi katika kufikiri na kuamua na kuusaidia mwili kutotumia nguvu kubwa hivyo kupumzika na kufanya mengine ila panapopaswa kutumika nguvu hakika nguvu itumike kwa kiwango cha kutosha kabisa kwani mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe.
Elimu ni muhimu sana katika kutatua changamoto zinazo mzunguka binadamu ingawa imekuja kupewa mtazamo (lengo) hasi (chanzo cha mtu kujipatia kipato pekee) na jamii ikiamini mtu akisoma lazima apate pesa tena za haraka ingawa kweli mtazamo huo sio mbaya maana kweli pesa ni muhimu na hata wengi hufuata elimu wakiwaza kujikwamua kiuchuni kwa ajira hukuu baadhi wakitamani pesa na maarifa kwa pamoja katika elimu ingawa pamoja na elimu nzuri pasipo nguvu na bahati mafanikio unaweza usiyapate kabisa katoka maisha kwani kuna nyakati vyote huitajika katika kujikwamua kimaisha.
Bahati ni muhimu sana kwani baada ya kutimiza wajibu wako wote bado kuna sehemu panahitajika bahati ili kuepukana na umasikini, ujinga na maradhi. Unapoelezwa kuna yai bovu moja kati ya mayai 10 mazima na uchague yai moja zima kati ya hayo mayai kumi na wewe kwa bahati mbaaya ukachagua bovu hapo unakua una kiwango cha chini sana cha bahati (mkosi au vijana husema `gundu’) na kila jamii ina namna yake inavyoamini vyanzo vya bahati na namna zinavyoweza kupungua, kuongezwa au kuibiwa kabisa, wapo wengi wanaokiri kabisa wanaishi maisha duni kwa kukosa tuu bahati kwani kuna wengi unawazidi vigezo lakini wanapata fursa mbele yako kwa bahati tu.
Pia unapoelezwa kati ya mayai kumi mayai tisa ni mabovu na yai moja ni zima uchague yai zima na wewe ukachagua yai zima moja katika tisa mabovu ukwel unakua una kiwango kikubwa cha bahati. Ukweli baada ya juhudi zote kuna sehemu panahitaji bahati.
Wapo wengi wamerithi mali nyingi na busara toka kwa wazazi wao huku wakiendeleza juhudi na maarifa katika maisha ila ukweli chanzo cha yote haya ni bahati tuu ya kuzaliwa familia yenye vyote hivyo kwani hatumia akili wala nguvu kufanya wazaliwe kwenye familia bora kwani ni ndoto za wengi kua katika familia za namna iyo ila huletwa kwa bahati sio nguvu wala akili huku wengine wengi wamezaliwa katika familia duni wakirithi umaskini wa fedha na elimu duni kwani familia zao duni hazikuweza kuwapa zaidi ya hayo na yote ni kukosa bahati ya kuzaliwa familia bora ingawa mwisho wa siku nguvu na akili inaweza kukunyanyua toka katika hali hio duni na kua katika maisha bora muhimu ni kutumia mtaji wa maskini ambao ni nguvu jumlisha akili nyingi kwani hata pasipo elimu binadamu amepewa akili za kutosha kukabiliana na mazingira yanayo mzunguka na pia mwishoni unaweza pata elimu ya mambo muhimu yatakayosaidia kutimiza malengo yako.
Mbaya zaidi wapo wenye maradhi sugu na ya kurithi ambayo bahati mbaaya waliyapata kwa bahati mbaaya au kurithi kwa wazazi wao ila ukweli wapo wengi wazima wa afya sio kwa akili zao wala nguvu zao ni kwa bahati tuu wapo salama kwani wengi hupita njia sawa na mwisho kua na matokeo pia tofauti.
Kuna msemo maarufu mtaani hususani kwa dada zetu kwamba usiringie uzuri ringia nyota, wakiwa na maana pamoja na uzuri wa msichana ila linapokuja swala la mahusiano bora au ndoa bahati inachukua nafasi kubwa zaidi kwani wapo wanaolewa ambao wamezidiwa uzuri na wengine wengi huku wengi wakiamini ndoa ni bahati tuuu ingawa ukweli tabia na mengine ni muhimu pia.
Kwa bahati mbaya kuna nyakati watu wengi hupunguza juhudi na maarifa huku wakitoa hoja kua hawana bahati na wengine wakikaa tuu wakisubiri bahati kwenye maisha jambo ambalo linachelewesha ndoto zao ingawa ukweli naamini bahati ina nafasi katika mafanikio.
Jaribu kutazama michezo ya kubahatisha ilivyopewa nafasi kubwa katika taifa letu huku watu wengi wakishiriki wakisubiri bahati iamue hatima ya maisha yao kwani huwezi tumia akili au nguvu kushinda mchezo wa bahati nasibu kwani mwenye bahati ndio hutajirika huku wengi waliokosa bahati wakibaki wakitoa kauli za kukata tamaa wakisema wamekosa bahati.
Hitimisho;
Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alibainisha maadaui wakubwa watatu wa maendeleo yetu yaani umaskini, ujinga na maradhi. Katika kukabiliana na maadui hawa lazima kutumia akili, nguvu na bahati. Hizi njia mbili (akili na nguvu) zimekua zikitumika kwa miaka mingi ila zote zimekua mwisho wa siku zinategemea bahati ili kukamilisha ukombozi kamili wa maisha ya wengi. Ukweli ni kwamba kufanikiwa kunasababishwa zaidi na uwiano sahihi wa nguvu, akili na bahati.
Panapo paswa kutumia nguvu kufanikisha jambo tumia nguvu ipasavyo ila muhimu kuhakikisha akili nyingi inatumika kupunguza matumizi mengi ya nguvu na pia jihadhari akili pekee sio njia sahihi ya kufanikiwa kwani kuna sehemu lazima kutumua nguvu nyingi na akili kidogo. Hivyo basi ni muhimu kutumia imani yako ipaswavyo kukabiliana na vyote vinavyoweza kuleta au kuzuia bahati ili uongeze nguvu na akili kukabiliana na hao maadui watatu na kupata mafanikio katika maisha.
Muandishi:
Whiteless Topson
Whitelesstopson@gmail.com
0763340113

Upvote
3