Akili Pekee Haitoshi. Kiwango cha Juu cha Akili ni Ufahamu

Akili Pekee Haitoshi. Kiwango cha Juu cha Akili ni Ufahamu

dgombusi

Senior Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
141
Reaction score
200
Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na akili na kuwa na ufahamu wa juu.

Watu wengi hufikiri kwamba akili (IQ) pekee inatosha kumfikisha mtu kwenye mafanikio, lakini ukweli ni kwamba ufahamu (awareness) wa hali ya juu

ndio unaotofautisha watu wa kawaida na wale wanaoweza kujitambua, kuelewa mifumo,
na kutumia maarifa yao kwa ustadi ili kupata wanachokitaka maishani.

Swali linakuja: Kwa nini baadhi ya watu wana ufahamu wa juu na wengine wa chini?

Tupe mtazamo wako!
 
Swali linakuja: Kwa nini baadhi ya watu wana ufahamu wa juu na wengine wa chini?
Tunaweza kugawanya watu katika makundi matatu kulingana na kiwango chao cha ufahamu.
  • Wale wasiojua wanachokifanya (Low Awareness)
  • Wale wanaojitahidi lakini wamenasa kwenye mfumo (Average Awareness)
  • Wale wenye ufahamu wa juu (High Awareness)
 
  • Wale wasiojua wanachokifanya (Low Awareness)
Hawa ni watu ambao maisha yao ni kama yanawaendesha.
Unakuta mtu anaishi mitaani, anaokota makopo, anaomba msaada au amekwama kabisa bila kujua afanye nini.
Wamekosa ufahamu wa hali yao na namna ya kutoka hapo.
 
Ni kweli kabisa,
Nature/Nurture.
inachangia, Kuna watu wanazaliwa na ufahamu wa juu, kisha wanakutana na mazingira na malezi ya wazazi wao.
Lakini unakuta mtu fulani haichukui muda mrefu kuelewa jambo, anajua namna ya kufanya jambo bila kufundishwa.
Anaweza kutazama kitu kwa haraka, akajifunza na kufanyia kazi kwa ubora zaidi kuliko mtu mwingine.
 
  • Wale wanaojitahidi lakini wamenasa kwenye mfumo (Average Awareness)
Hili ni kundi kubwa la watu. Wanaweza kuwa na kazi, biashara au elimu fulani, lakini bado hawaelewi kikamilifu jinsi mfumo unavyofanya kazi.
Wanahangaika ndani ya maisha lakini hawana uwezo wa kudhibiti mazingira yao kwa kiwango cha juu.
 
kijifunza.bila kujifunza huwezi kuwa na ufahamu wowote.
Ni kweli kabisa, kujifunza ni muhimu sana ili kupata ufahamu.

Bila kujifunza, ni vigumu kuwa na ufahamu wa juu na kuelewa mambo kwa kina.

Hata hivyo, fact ni kwamba kuna watu wanazaliwa na ufahamu wa juu na hawatumi nguvu kubwa kwenye kujifunza,
lakini bado wanaelewa mambo kwa haraka na kwa kina.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na akili na kuwa na ufahamu wa juu.

Watu wengi hufikiri kwamba akili (IQ) pekee inatosha kumfikisha mtu kwenye mafanikio, lakini ukweli ni kwamba ufahamu (awareness) wa hali ya juu

ndio unaotofautisha watu wa kawaida na wale wanaoweza kujitambua, kuelewa mifumo,
na kutumia maarifa yao kwa ustadi ili kupata wanachokitaka maishani.

Swali linakuja: Kwa nini baadhi ya watu wana ufahamu wa juu na wengine wa chini?

Tupe mtazamo wako!
1.Genetics,.......kama tu ilivo wewe una mkono mkubwa ama mdogo,una rnagi tofauti na mwenzako basi hata Emotional intelligence yako wewe na wengine inatofautiana
2.Mazingira
Kuna mtu anazaliwa na kulelewa na walezi walio na ufahamu mkubwa mno wa maisha anajikuta anaadapt
3.Shule,Vyuo........kama Kibaha,Mzumbe,Ilboru,Feza,.....IST etc,Wanawaitrain wanafunzi wao kua above average,kuthink above the border,...........vyuo kama Harvard,Stanford etc vinafuata hio njia,Kwa bongo vyuo vingi ni sehemu za kukalili TU
 
Mtu akiwa na IQ kubwa halafu akawa na roho ya panya ana feli maisha. Simple

Ufahamu wa mtu unatokana na Uzoefu, Mazingira/Matukio, Interest

Now vijana wengi wamekua addicted na kuwa machawa
 
1.Genetics,.......kama tu ilivo wewe una mkono mkubwa ama mdogo,una rnagi tofauti na mwenzako basi hata Emotional intelligence yako wewe na wengine inatofautiana
2.Mazingira
Kuna mtu anazaliwa na kulelewa na walezi walio na ufahamu mkubwa mno wa maisha anajikuta anaadapt
3.Shule,Vyuo........kama Kibaha,Mzumbe,Ilboru,Feza,.....IST etc,Wanawaitrain wanafunzi wao kua above average,kuthink above the border,...........vyuo kama Harvard,Stanford etc vinafuata hio njia,Kwa bongo vyuo vingi ni sehemu za kukalili TU
Mazingira yanamchango mkubwa sana katika maendeleo ya akili na ufahamu.

Kama vile ulivyosema, genetics inaweza kuathiri kiasi fulani, lakini mazingira, malezi, na shule pia vina mchango mkubwa.

Kuna watu wanaozaliwa na ufahamu wa juu lakini mazingira na walezi wao wanaweza kuathiri jinsi wanavyoweza kuufanya ufahamu huo kung'aa.
 
Back
Top Bottom