Akili si ya kuhifadhi wazo, bali ya kubuni wazo

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,278
Reaction score
956
TAFAKURI …. AKILI SI YA KUHIFADHI WAZO, BALI YA KUBUNI WAZO.

Unatoka kazini ukiwa na mambo mengi kichwani . Ghafla unakumbuka unatakiwa kupitia kitu muhimu nyumbani . lakini unasema nikifika tu nyumbani nitamtuma mtoto akanunue .

Lakini unapofika nyumbani unakumbana na vitu vingine tena vingi . Aidha kuna taarifa na majukumu ambayo yanakutoa katika mstari . Hadi kesho au baada ya muda Fulani ndipo unaanza kukumbuka tena . Sababu kubwa ni kutopangilia ipasavyo . HUNA UTARATIBU NA RATIBA YA MAMBO YAKO . Wewe unataka kukumbuka kila kitu . Jambo hili si la kawaida na haliwezekani . kumbuka vitu kwa vipaumbele vyake na utaratibu uliouweka .

Kazi ya akili yako ni kufikiri , kufanya maaumuzi na kutatua matatizo . hauendi zaidi ya hapo na si kuhifadhi tu . Akili imetengenezwa kuleta ubunifu . ndiyo maana albert Einstein alikuwa hafahamu namba yake ya simu . Alipoulizwa yeye alisema , mimi ninayo katika phonebook , ni swala la kungalia na kupiga . Kwani akili yangu ni ya kubuni na si kuhifadhi . Mind is not for storing idea ,but is for creating ideas.

Tunaishi katika dunia ambayo vitu vingi sana vinaingilia maisha yetu na mipango Yetu . Kuna matumizi ya simu , tv , nk . Hata tunafika mahli tunakosa control ya maisha yetu wenyewe .

Hapa ndipo unapopata sheria ya Bwana david allen,( GTD ) Getting things done . Huu ni utaratibu wa mawazo namna ya kupangilia mawazo yako ili upate uzalishaji chanya katika mradi wako . Fanyia kazi jambo kwa mujibu wa uwezekano wake , na kama ulivyopanga . Akili yako ni kwa ajili ya kukamatia mawazo( to capture a thougth) , si kuyashikilia( not To hold them). Akimaanisha ukishikilia mambo lazima yakuponyoke .

Kama akili yako ikiwa inapanga mambo kwa mpangilio sawia utapata matokeo chanya . Akili yako inakusaidia kuweka record na utaratibu wa majukumu , kipi kianze na kipi kifuate . SI KUHIFADHI TU .

Katika utaratibu huu wa GTD Kuna hatua tano za kufanya mambo yatokee .

. 1 - Capture 2 - Clarify 3 - Organize 4 - Reflect 5 - Engage

Kitu cha kwanza ni kukamata kwanza jambo lolote aidha inaweza kuwa ni taarifa . Unatakiwa kukamata na si kuingiza tu katika akili yako bali kukusanya kwa ajili ya hatua ya pili . taarifa zozote zinazotoka kwa watu zinaweza kuwa ni wazo la kuzaa shughuli kwako . ZIKAMATE KWANZA ( CAPTURE THEM) . Hapa ndiyo wengi tunakamatwa , kwani kukamata tunakamata . Tunafanyia nini , ndiyo kazi ilipo.

Baada ya hatua hiyo unatakiwa uanze sasa kujiuliza je inawezekana ( is it actionable ) . Jibu katika taarifa yote hiyo itakuwa YES or NO . hapa kuna mchujo . Hata jibu likiwa ni ndiyo ,lazima uangalie itachukua muda gani kutenda . Kama itakuwa ni hapana , lazima utenge na kuliweka kwa angalizo la ziada , unaliacha kwa muda au kulitupa kabisa . Utafanya hivi kwa kila hatua za taarifa ulizo nazo .

Baada ya kuchakata ni wakati wa kupangilia . Hapa tunapata mpangilio katika jambo husika , muda na maudhui yake . Vitu vya aina moja lazima uviunganishe pamoja , usivitenge . vile vinavyohitaji muda maalum navyo lazima viungane pamoja . kuna vingine aidha vinahitaji aidha kufanywa na mtu mwingine hapa ndiyo mahali pa kuamua .

Swala kubwa hapa ni namna ya kuchukua zile hatua , kipi kianze na kipi kisianze . Mimi natumia one note kwa computer na keep note kwa simu . Inanisaidia sana principle hii .sina takataka kichwani na mlundikano wa majukumu kichwani .

Baada ya hapo , fanya rejea ya vile ulivyopanga . kama ulikuwa unajua kuna sehemu hukufanya sawa ni wakati sasa wa kurudia , unaweza kufanya kila baada ya muda Fulani . Kama una mipango mikubwa jiwekee utaratibu wa kurejea mambo yako kila baada ya mwezi .

Baada ya hapo unaenda kufanya .kama taarifa unazo nyingi inabidi na akili inatakiwa kuwa katika hali ya UKUU . Yaani akili kubwa tatizo kubwa akili ndogo akili ndogo katika kutatua . kwa kufanya hivyo kila kitu kitakuwa kimekaa mahali pake na hakuna cha kukuponyoka tena , na hutakuwa mtu wa kupoteza muda . Mambo mengi yatapata kufanyika .

Watu wengi hapo wanapanga , Lakini kwa mkusanyiko wa taarifa nyingi kichwani . wanajikuta kwa kuwa hawaweki mtiririko huu wanakwama . Wanahudhuria semina nyingi na hakuna matokeo .

Biblia inasema .Mithali 21:5 ,.’’’ Mawazo ya wenye bidii huelekea utajiri tu ; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji .’’’’’( ESV BIBLE) . The plans of the diligent lead surely to abundance, but everyone who is hasty comes only to poverty.

TAFAAKRI NAMI
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…