Jamani,mimi naamini kujifunza hakukuishia darasani,na sipendi kufanya mambo kimazoea.Kuna hii kitu nimekua nikisikia tangu mdogo,AKILI.Je ni nini?Je ni ufahamu?Inapimwaje?Shule kwa mfano,yule anaefaulu masomo huonekana ana "akili" lakini ukija mtaani unamkuta ni mlevi,mnyanyasaji,mkatili,mpenda fujo n.k,je huyu kweli ana akili?Au ubongo ni akili?Nijuavyo mimi ubongo ni kifaa anachotumia mtu kufikiri.Sasa akili iko wapi?Inakaa mwilini?Je ni eneo lipi inakaa?Au ufahamu ndio akili,Kama ni ndio ufaham ni akili?Hebu fungukeni mtusaidie sisi wenye kutanzwa na hii kitu!
Iron Lady
tatizo ni negative sikuzote hakuna tatizo positive lady
mkuu qualified,
si kama katika hesabu wanasema problem find solution hivyo sio tatizo kwa maana ya negativity ya kitu hicho ila kwa vile inahitaji solution.nilikuwa namaanisha hivyo mkuu
Kwa uelewa wangu akili ipo, ila haionekani(invisible) na (haishikiki)untoucherble. Akili inapimwa na inakuwa kadri mtu anavyo kuwa. "IQ" inteligence of quotent, ni kipimo cha ufahamu. Mtoto huwa anazaliwa na IQ 0 kama ilivyo kwa nyani. Kila siku anavyozidi kukua ndo akili yake inavyozidi kukua. Mtu mwenye IQ Kubwa ni 1700. Tafauti ya binadamu na nyani ni kuwa nyani IQ yake inaanzia 0 inaishia 500. Angefanikiwa kufikisha iq 700 angeweza kuongea angalao kama mtoto,angeweza kuita maji mma! Mtu mzima, wengi wanaufahamu wa IQ 1500-1600 wale wenye ufahamu mkubwa wana IQ 1750. Mtu ukifikisha miaka 70 na kuendelea kulingana na mabadiliko ya mwili, IQ yako inaanza kudumaa!
HATA MIMI HUWA NAJIULIZAGA SANA KUHUSU AKILI/IQ
Huwa najiulizaga pia Mtu akiwa na uwezo mkubwa wa kukariri, hiyo ni akili?
Mtu akiwa anafanya mambo ya hovyohovyo (comedian) akawafurahisha watu huyo ana akili au IQ kubwa?
mtu akiwa ***** au wa mwisho darasani lakini anaujuzi juu aina fulani ya mchezo au ufundi, ana akili au IQ kubwa?
Mtu akiwa bingwa wa kuwaimbisha mabinti (tongoza) na kufanikiwa , ana akili au IQ kubwai?
Mtu akiwa na elimu kubwa (PhD in Business) halafu hawezi kufanya biashara ,huyo ni bwegeee hana IQ kubwa?
Akili ni nafsi isiyoonekana ambayo huboreshwa kwa vichocheo vingine kama kufikiri au kutafakari na kutenda ili kupata matokeo yanayoweza kuwa mazuri au mabaya. Akili huendana na kufikiri,udadisi,ufahamu,uelewa,umakini na utulivu. Mara nyingi mtu akifikiri vizuri na kutenda yaliyosahihi na matokeo yake kuwa mazuri,mtu huyo atasemwa ana akili.
Mtu asiye mgonjwa,ghafla akatenda kitu cha ajabu kama walivyofanya askari kumpiga na mmoja wao kumwua mwandishi wa habari Daudi Mwangosi na kujutia kitendo chake hicho cha kinyama baadaye, mtu huyo atasemwa hana akili timamu. Akili ni uwezo wa kufikiri na kutenda kwa ufanisi.Lakini bado matokeo ya kufikiri na kutenda yanaweza kuwa chanya au hasi.
Hii TOPIC imeniweka njia panda, unajua huku mtaani kwetu kuna jamaa
ana matatizo ya akili. Yaani ana uchizi hasa tena kaishia Form II Pamoja
na uchizi wake anapoingia kwenye mchezo wa draft anaogopwa sana yaani
akili yake ni kubwa katika kulicheza draft. Si draft tu hata bao ambalo linahitaji
akili na hesabu za haraka, kweli inashangaza hii akili ni nini?
Don't mix up Intelligence and smartness!Not every smart person is intelligent