Akili . . . . . !!!!

Mental age na kalendar age weka sawa tupige mahesabu, zifafanue tujiculculate
 
Mkuu hili swali la Akili ni nini linakanganya sana.
Naomba nijibu kwa uelewa wangu finyu au uelewa wenyewe ndio Akili? Wataaramu wengi wanasema akili tunazaliwa nazo ila tunachoongeza ni ufahamu na kutofautiana ni huo Huo ufahamu ndio maana kuna levo tofauti kwenye taaruma moja.
Akili ni jinsi unavyochanganua mambo kwa uelewa mpana ndio maana kuna watu hawajasoma lakini mahakama inawaita kushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Ukiweza kubuni jambo liwe ni biashara,afya na chochote kile kitakachoweza kutatua shida za jamii wewe= una akili

2. Ukiweza jikuta uko kwenye misukosuko ya kimaisha isiyo na ufumbuzi wa mtu mmoja peke yake lakini wewe ukaweza kujitatulia shida hiyo bila msaada wa mtu mwingine wewe= una akili

3. Kitendo cha kuandika vitabu vikatumika kufundishia watu mashuleni au mitaani na wakabadilisha maisha yao kupitia uwezo wako wewe= una akili

4. Ukipiga kitabu kama CP na ukawa mkaguzi wa mahesabu magumu,au ukapasua Sayansi mpaka tukastukia tukija hospital unatupasua kichwa na kutuludishia tena uhai na jinsi tulivyokua awali wewe= una akili

Kiufupi ni kama hivyo kwa uelewa wangu

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Mjadala ni mzito kweli kweli.
Naona tunachangia matokeo ya kazi ya akili hatujafikia lengo la swali.

Akili ni nini?????
 
Jibu lako tosha kabisaaa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili ni "zao" la ubongo. Ubongo ukiwa na uwezo wa kutafakari na kupambanua changamoto zinazojitokeza na kupata ufumbuzi safi/chanya (na huenda hata ufumbuzi chanya wewe kwa maksudi ukatenda hasi) wewe bado utaitwa mwenye AKILI. Mtu anaweza kuwa bingwa wa Accounts, kwa mfano, akatumia akili hiyo KUIBIA umma. Mtu huyu atakuwa ametumia akili yake iliyotukuka kwa mtazamo hasi. Dhana hii ni tofauti na ule msemo wa wahenga kuwa AKILI NYINGI HUONDOA MAARIFA!
Huu ni mtazamo wangu tu.....

Nawakilisha
 
Jamani nami naomba nichangie kama ifuatavyo, mnataka kusema wanyama hawana akili? sidhani akili wanazo ila tumewazidi ufahamu, akili imetokana na ubongo, ubongo unaonekana akili haionekani ila akili tunaitafsiri kwa sababu tuna ufahamu, kwenye ufahamu ndipo tulipowazidi wanyama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…