Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Moja kati ya mambo ninayopenda katika kupika ni ile raha na furaha ninayopata pale ninapotengeneza recipe mpya ya chakula na ikapendwa na wale waliokula chakula hicho.
Pancakes si chapati maji kama wengi waaminivyo,Ni mapishi mawili tofauti katika mahitaji yanayotumika,mbinu za uchanganyaji na ukaangaji wake.
Ingawa nimepika pancake kwa miaka mingi,sikuzote nimepika kwa kutumia recipe ya mtu Fulani.Lakaini recipe hii ninayokupa leo ni yakipee zaidi,ni recipe yangu binafsi ambayo imebeba mjumuiko wa mbinu na kanuni mbalimbali za upishi ili tu kukupa wewe kilicho bora zaidi
Mahitaji
Andaa pancake hizi asubuhi mapema kabla moto wowowte haujawashwa jikoni,
lengo nikuhakikisha hakuna joto jikoni kwani joto huaribu matokeo mazuri ya pishi hili
Njia
1.Changanya unga na baking poda kisha chekecha kwa pamoja.
Lengo nikuruhusu unga upate oxygen nyingi ili utengeneze nafasi za hewa wakati wakukaanga
2.Katika bakuli ya kioo,udongo au plastiki weka ute wa mayai na sukari,changanya pamoja adi mchanganyiko wote uwe povu
4.Weka kikaango jikoni katika moto mdogo,kikishika moto ,weka mchanganyiko wa unga kisha tumia kitako cha kijiko kusambaza unga nakutengeneza uduara upendao. Acha adi uone kama matundu ya hewa yanatokea juu ya pancake,weka mafuta kuzunguka pancake kwa nje,kisha geuza ili kuivisha upande wa pili,weka mafuta tena kuzunguka pancake kwa nje,ikiiva huwa na rangi ya dhahabu.Fanya hivi adi unga uishe.
Pancake zikiwa tayari acha zipoe kisha nyunyuzia pancake syrup au asali juu yake pale unapotaka kula.

- Mayai 5- tenganisha kiini na ute kwenye bakuli mbili tofauti
- Sukari vijiko 2 vya chakula- Sukari hutumika kidogo ili kueuhusu matumizi ya cyrup/asali
- Unga wa ngano vijiko 8 vya chakula
- Baking poda vijiko 3 vya chai
- Maziwa nusu kikkombe -tumia maziwa ya unga,changanya nusu kikombe cha maji baridi (very cold water) na vijiko 3 vya chakula vya maziwa ya unga.
- Mafuta ya maji –si zaidi ya 1/2 kijiko cha chai kwa kila pancake/mafuta kidogo kadri uwezavyo
- Pancake syrup au asali kwakiasi upendacho
Andaa pancake hizi asubuhi mapema kabla moto wowowte haujawashwa jikoni,
lengo nikuhakikisha hakuna joto jikoni kwani joto huaribu matokeo mazuri ya pishi hili
Njia
1.Changanya unga na baking poda kisha chekecha kwa pamoja.
Lengo nikuruhusu unga upate oxygen nyingi ili utengeneze nafasi za hewa wakati wakukaanga
2.Katika bakuli ya kioo,udongo au plastiki weka ute wa mayai na sukari,changanya pamoja adi mchanganyiko wote uwe povu
- Epuka kutumia chambo cha chuma au bati kwani hunyonya joto kwa haraka nakufanya ute wayai uwe mzito ,uzito huo ufanya ushindwe kupata povu linaloitajika
- Weka bakuli ndani ya friji ili liwe baridi sana kabla yakutumia
- Unga na maziwa huongezwa kwa kidogo kidogo ili kutoa nafasi yakuchanganya na kulainisha unga pasipo kutengeneza mabonge.
- Hakikisha kua kiini cha yai ni kitu chamwisho kabisa kuweka katika mchanganyiko huu.
4.Weka kikaango jikoni katika moto mdogo,kikishika moto ,weka mchanganyiko wa unga kisha tumia kitako cha kijiko kusambaza unga nakutengeneza uduara upendao. Acha adi uone kama matundu ya hewa yanatokea juu ya pancake,weka mafuta kuzunguka pancake kwa nje,kisha geuza ili kuivisha upande wa pili,weka mafuta tena kuzunguka pancake kwa nje,ikiiva huwa na rangi ya dhahabu.Fanya hivi adi unga uishe.
- Usitangulize mafuta kwenye kikaango kabla hujaweka mchanganyiko wako nakuusambaza,ukifanya hivyo hutaweza kuipa pancake umbo zuri kwani mafuta hufanya unga utereze kwenye kikaango.
- Usikaange kama chapati maji au chapati za kusukuma, tumia kanuni hii iliyoelekezwa hapa kwa matokeo mazuri.