Akimz Elli anasema "MIMI SIO MNYONGE"

Akimz Elli anasema "MIMI SIO MNYONGE"

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Hivi ni kwa nini ung'ang'anie kutwita sisi "wanyonge" tena kwa kujigamba, eti; mimi ni rais wa wanyonge"
Nani kakwambia sisi ni wanyonge? Una ajenda gani ya siri kutung'ang'aniza tuwe wanyonge?
Weee!? Shika heshima yako. Sisi sio wanyonge. Anyway, naji sema mwenyewe. Kwa kweli mimi sio mnyonge. Na kwa nini niwe mnyonge!? Hivi wewe; mimi si ndio nilikupigia kura ukapata hilo gepu la uongozi? Na wakati unaniomba hilo gepu uliniomba kwa unyenyekevu mkubwa! Nilikupa gepu na mara leo umekuwa mjanja unaniona mimi fala na unaniita "mnyonge".
Aah! Hata! Siwezi kukubali, mimi sio mnyonge bwana. Na kwa nini niwe mnyonge?
Kuna siri gani kwenye kunilazimisha niwe mnyonge?
Kama na wewe unaesoma hii post unaamini sio mnyonge mkatalie katu katu, mwambie live; hapana mzee mimi sio mnyonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
neno linaposemwa halafu halikuhusu huwezi ukaumia hata kidogo kwa nini
niteseke sasa na yasiyonihusu!!
mnyonge lazima Uteseke sana linaposemwa hilo neno. hakika wewe bado ni mnyonge .

Mimi ni mtanzania mwenye nguvu na akili timamu.
 
neno linaposemwa halafu halikuhusu huwezi ukaumia hata kidogo kwa nini
niteseke sasa na yasiyonihusu!!
mnyonge lazima Uteseke sana linaposemwa hilo neno. hakika wewe bado ni mnyonge .

Mimi ni mtanzania mwenye nguvu na akili timamu.
Hapa "anajenerolaizi" yaan wote ni wanyonge?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom