kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Tulimuondoa Muhidini Ndolanga na Rage kwenye mpira kwakuwa mambo ya mpira yalikuwa hayaendi vizuri nchini. Tulidhani sababu ni kwasababu akina Ndolanga na wenzake hawatoki kwenye familia ya mpira wa miguu hivyo hawajui kuongoza mpira. Hivyo watanzania tukaaminishwa kuwa tukiwaweka viongozi waliowahi kuucheza au kuuongoza mpira mambo yetu ya soka yatakwenda vizuri na makombe tutapata.
Tangu waondoke akina Ndolanga na wenzake na kuwakaribisha "football family" hali yetu imebaki ileile au heri ya akina Ndolanga. Akina Mzee Tenga, Malinzi na sasa Karia mambo yetu ni yaleyale tu ya kichwa cha mwenda wazimu.
Kuna haja ya kuwaomba radhi akina Ndolanga na Rage kwanza kwa kejeli tulizowapa kabla ya kutafuta chanzo halisi cha kuboronga kwetu kwenye mpira.