Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Sakata la yule Afisa wa TRA aliyefariki limeendelea kuchukua sura mpya.
===================
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda, ametangaza kuwa oparesheni zote za kitengo cha Fast cha kudhibiti wakwepa kodi zitafanywa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuanzia sasa.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya tukio la kusikitisha la kuuawa kwa dereva wa TRA, Amani Kamguna Simbayao, aliyeshambuliwa na wananchi wakati wa utekelezaji wa majukumu yake katika eneo la Tegeta Nyuki, Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu, Bw. Mwenda amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwakamata washukiwa wa tukio hilo na amesisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Amefafanua kuwa gari lililokuwa likifuatiliwa na marehemu na wenzake liliingizwa nchini kwa njia za magendo bila kulipa kodi, na kodi hiyo ingeweza kuchangia maendeleo ya taifa.
"Ningependa mjue kwamba kazi wanayofanya watumishi wa TRA ni kwa niaba ya Watanzania wote. Marehemu Amani alijitahidi kuhakikisha kodi inakusanywa ili kuboresha maisha ya wananchi. Hatustahili kuona wafanyakazi wa TRA wakifanyiwa matendo kama haya. Wanastahili heshima kwa kazi yao kubwa," amesema Bw. Mwenda.
Bw. Mwenda aliendelea kusema kuwa TRA itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kodi na mamlaka ya watumishi wake katika kutekeleza majukumu yao.
"Kwetu sisi, Marehemu ni shujaa wa taifa. Alifariki akiwa kazini, akilinda mali ya serikali kwa uadilifu na uzalendo mkubwa. Hatutamsahau kwa mchango wake mkubwa," amesema Bw. Mwenda.
Akizungumzia familia ya marehemu, Bw. Mwenda ameahidi msaada wa kiuchumi na kijamii.
Source: Jambo TV