Akiwa na Miaka 31 Chama ni sawa na Domayo

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Baada ya mechi ya Mtibwa niliweka uchambuzi wangu humu kumhusu CHAMA.

Niliweka wazi kuwa CHAMA amebakiza jina tu na wala hana uwezo wa kucheza LIGI KUU BARA kwa ufanisi tena.

Umri umemtupa, Ushindani kwenye Ligi Umeongezeka.

Ujio wake uliongeza zaidi idadi ya wachezaji wenye miaka 31 na kuendelea.

Sasa anaishi kwa pressure kubbwa sana kutoka kw amashabiki wanao mtaka awe anafunga magoli kama enzi zile. Enzi ambazo kimtazamo zilikuwa za mwisho katika maisha yake ya soka.

Wapo walionibeza na wapo wengine walio nyanyua hata simu zao kunipigia na kunishambulia kwa uchambuzi wangu.

Kuna waliosema kuwa Chama hakuonyesha kiwango kwa sababu ya maji uwanjani. Sasa je na pale Kaitaba kulijaa maji?

Simba hatokuja twaa Ubingwa wa LigiKUU akiwa na CHAMA, BOCCO, MUGALU, KAGERE na KAPOMBE.

Inabido hiko kizazi kiondoshwe mapema ili kuwepo na nafasi kwa ajili ya damu mpya.

- Bela Ciao -
 
Umeangalia mpira vizuri kweli wewe au ndo wale msioelewa ata majukum ya wachezaji uwanjani yakoje. Chama kwa mfumo ulivyokua kacheza vizuri kwahiyo swala lakutofunga hayo sasa ni mapungufu ya timu nzima ilivyocheza na mipango ya mwalimu ilivyokua.kama uelewi uliza usaidiwe.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Baada ya mechi ya Mtibwa niliweka uchambuzi wangu humu kumhusu CHAMA.

Niliweka wazi kuwa CHAMA amebakiza jina tu na wala hana uwezo wa kucheza LIGIKUU BARA kwa ufanisi tena...
Mimi ngajapo nitaendelea kukubeza sana na kuona wewe ni punguani wa akili!! Kwani kushindwa kwa simba Leo ni kwa sababu ya chama kupungua kiwango? Acha uongo..nasema Acha uongo....

suala la simba kwa sasa ni sikio la kufa... timu nzima haiko vizuri.....chama kacheza vizuri kabisa... tatizo ni kwamba akili yako yote ulikuwa unamfikiria chama na ulijiandaa uandike chochote kuhusu chama mara tu baada ya match kuisha.
 
Timu yetu Simba haiko sawa lakin kwa hili la chama ntakupinga Sana tu pia inaonyesha wewe hujui mpira na majukumu ya kila mchezaji.
Sijaona chama Kama kacheza vibaya ,leo chama kakiwasha sana tu Tena alikuwa anacheza pemben wakat yeye Ni no 10 ,Sijui ulitaka afunge ndio ujue chama Bado Ni super kabisa au Ni vipi.

Ifike wakat kabla hatujacomment hapa tufuatilie takwimu na jukumu la kila mchezaji ,hata misimu iliyopita chama hakuwa mfungaji wa kiwango hicho ulichokisema Zaid chama Ni mtengeneza pass na Leo kafanya hivyo ,Sasa bila forward ya kueleweka Nan angefunga?

Je Ni nafas ngapi zimetengenezwa na wameshindwa kuzitumia?

Ungekuja na swala la kutokuwa na finishers wazur hoja yako ingekua na mantiki lakin hili la chama naona Kuna chuki binafsi tu dhidi ya chama.

Chama hawez kuwa mtengeneza pass ,wakat huo huo awe forward ,wakat huo huo awe beki ,so kila mchezaji Ana jukumu lake uwajan.

Bahat mbaya bongo ushabiki wa Simba na yanga umetuharibu Sana Tena Sana .
 
Chama kacheza vizuri sana labda kama kuna kingine unatafuta na pia Chama sio striker mpaka tumlaumu kwanini hafungi...jukumu lake ni kiungo na kiungo kazi yake ni kuwapatia mipira ya mwisho washambuliaji(striker) ndio maana ata msimu 2018/19/20 aliongoza kwa assist na kagere,bocco wakaongoza kwa mabao

...unaweza kufatilia Kulfi au Juakali mpira amna kitu unajua mkuu

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Timu yetu Simba haiko sawa lakin kwa hili la chama ntakupinga Sana tu pia inaonyesha wewe hujui mpira na majukumu ya kila mchezaji.
Sijaona chama Kama kacheza vibaya...
Mkuu , Tanzania kwa sasa ina Mashabiki na wachambuzi wa ajabuajabu tu. Kwa mawazo ya mleta uzi , alitaka kila mpira chama auguse. Mpira ukielekea langoni kwake chama ageuke kuwa kipa audake. Kwa kifupi alitaka chama awe ndiye uwanja wa mpira , kila mpira ukidunda udunde kwakwe .
 
Timu yetu Simba haiko sawa lakin kwa hili la chama ntakupinga Sana tu pia inaonyesha wewe hujui mpira na majukumu ya kila mchezaji.
Sijaona chama Kama kacheza vibaya...
Halafu lile boko la goli la kiiza katoa chama ila mikia mnajifanya kama amkuona vile!
 
2021 - Kila mchezaji Simba alikuwa mzuri
2022 - Wachezaji wote Simba ni wabovu

Hahah, kutuelewa mashabiki wa bongo inahitaji digrii...
 
Kwa mfumo wa mechi ya leo kulikua hakuna natural striker hivyo magoli yalitakiwa yatoke kwa viungo
 
Timu yetu Simba haiko sawa lakin kwa hili la chama ntakupinga Sana tu pia inaonyesha wewe hujui mpira na majukumu ya kila mchezaji.
Sijaona chama Kama kacheza vibaya...
Halafu lile boko la goli la kiiza katoa chama ila mikia mnajifanya kama amkuona vile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…