Al Ahly wagombea mechi yao ya daby na Zamalek.

Al Ahly wagombea mechi yao ya daby na Zamalek.

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Moderator, Paw 255Fixer , kichwa Cha habari kisomeke Al Ahly wagomea mechi ya dabi dhidi ya Zamalek.

Klabu ya Al Ahly imegoma kushiriki mechi yao ya dabi dhidi ya Zamalek ikisisitiza kuwa Shirikisho la Soka la Misri (EFA) linapaswa kuteua mwamuzi wa kigeni badala ya kutumia waamuzi wa ndani. Ahly imetishia kujiondoa kwenye Ligi Kuu ya Misri endapo ombi lao halitatekelezwa.

Dabi hiyo ilikuwa sehemu ya hatua ya mbio za ubingwa lakini EFA ilitangaza usiku wa kuamkia Jumanne kuwa mchezo huo utasimamiwa na waamuzi wa ndani, kinyume na makubaliano ya awali na kufuatia mkutano wa dharura uongozi wa Ahly ulitoa tamko rasmi ukitaka mchezo huo uahirishwe hadi mwamuzi wa kigeni apatikane.

Ahly ilisisitiza kuwa iliwasilisha maombi yake mapema, ikitaka waamuzi wa kigeni kwa mechi muhimu ili kuhakikisha haki inatendeka, hasa baada ya makosa ya mara kwa mara ya waamuzi wa ndani. Hata hivyo, EFA ilijibu ikidai muda haukutosha kuwapata waamuzi wa nje na kuitaka Ahly kuunga mkono waamuzi wa ndani.

Mpaka sasa, EFA haijatoa tamko jipya, huku hali ya sintofahamu ikiendelea. Katika msimamo wa ligi, Pyramids FC inaongoza kwa alama 42 Ahly ikiwa ya pili na 39 huku Zamalek ikishika nafasi ya tatu kwa alama 32.
 
Al ahly kama utopolo wazee wa kulialia
 
na kwa ustawi wa soka la tanzania inabidi siku za usoni tulifikirie litasaidia kuondoa mikanganyiko kwenye uamuzi.
 
Wakubwa wa africa Simba na Al Ahly wameamua kukataa mambo ya kihuni kwenye soka

Kitaeleweka tu

Mpaka mrudi kwenye misingi ya Soka
 
Bora hata hao wamesusia kwa sababu walikuwa wana makubaliano yao kuhusu mwamuzi wa kigeni kuchezesha hiyo mechi yao! Huku kwetu kuna timu imeogopa kucheza mechi, kisa tu baadhi ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ni majeruhi.
 
Wawinda mbuzi utawajua tu
 
Bora hata hao wamesusia kwa sababu walikuwa wana makubaliano yao kuhusu mwamuzi wa kigeni kuchezesha hiyo mechi yao! Huku kwetu kuna timu imeogopa kucheza mechi, kisa tu baadhi ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ni majeruhi.
Ni kujitoa ufahamu kuliko pitiliza mkuu kama haya ndiyo mawazo yako na uwezo wako wa kufikiria umeishia hapo.

Simba alitoa sababu zake kwamba wamezuiliwa kufanya mazoezi kinyume na kanuni zinavyotaka.

Bodi ya ligi pia kwenye press release yao walisema sababu ya kuahirisha mechi ni kutokana na Simba kuzuiliwa kufanya mazoezi sasa wewe unapokuja na mawazo yako ina maana unajua zaidi kuliko Simba na Tff?
 
Back
Top Bottom