Tetesi: Al Ahly wanamtaka Ronaldo kwa mkopo wa miezi sita kwa ajili ya Kombe la Dunia la Vilabu Marekani

Tetesi: Al Ahly wanamtaka Ronaldo kwa mkopo wa miezi sita kwa ajili ya Kombe la Dunia la Vilabu Marekani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Inaelezwa kuwa Wajumbe wa bodi ya Al Ahly wamependekeza kwa Rais wa klabu hiyo, Mahmoud El Khatib, kujaribu kumsajili Cristiano Ronaldo kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu litakalofanyika nchini Marekani.
IMG_1464.jpeg
IMG_1463.jpeg
Baada ya kuweka rekodi ya mabao kwenye Ligi Kuu ya Saudi Arabia msimu uliopita, Ronaldo ameendelea kwa mwanzo mzuri katika msimu wa 2024/25. Kufikia Desemba 7, 2024, amefunga mabao 16 katika mechi 19 za mashindano yote akiwa na Al Nassr.
 
Ronaldo sio hela tu anahitaji bali hata heshima na kujitunzia hadhi nd mana anakataaga hata baadhi ya kusajiliwa vilabu ulaya kisa vipo europa. Ronaldo kucheza Africa!!! "ngumu"
 
wabongo naona hawajaelewa hii habari, Al ahly wanataka January wamchukue ronaldo kwa mkopo miezi 6 ili awasaidie kucheza Fifa club world cup kwa hivyo mkataba wake utaisha Mwezi wa 7 ambapo Club world cup itakuwa inaisha.... na yeye ataludi zake Al nassr,

Kwa kufupisha ni kwamba hata akisajiliwa January hatoruhusiwa kucheza Caf kwakuwa amesajiliwa dirisha dogo, ila Ligi la Misri ataruhusiwa kucheza na tujikumbushe Ligi la misri lina ushindani na ubora kuliko hata Lile Saudi pro League.
 
Hela ya kumlipa hawana, halafu CR7 ukiachana na uwezo aliokuwa nae pili ni brand kubwa mno.
 
Hela ya kumlipa hawana, halafu CR7 ukiachana na uwezo aliokuwa nae pili ni brand kubwa mno.
Hela wanayo ndomaana wamemtaka na pia ujio wa Ronaldo tu utawaletea Wafuasi na Deal za biashara nyingi ambazo zitarejesha Faida ndani ya Mwezi tu....kuanzia Mauzo ya Jezi, Haki miliki za mechi zao, Gate collections, Insta Followers, Deals za Nike/Adidas zitapandishwa Dau kwa upande wao nk....
 
Ronaldo sio hela tu anahitaji bali hata heshima na kujitunzia hadhi nd mana anakataaga hata baadhi ya kusajiliwa vilabu ulaya kisa vipo europa. Ronaldo kucheza Africa!!! "ngumu"
Anacheza wapi sahivi
 
Mshahara wa Cr7 kwa miezi 6 unazidi/unakaribia kuzidi thamani ya vilabu vyote Afrika kwa pamoja vilivyo CAF CL & CAF Confederation cup.

Analipwa takribani bilion 350 za kitanzania kwa miezi 6 hapo haujagusia bonus na mazagazaga mengine.
Hivyo kwa miezi 6 huenda anaokota kama Tsh 500B.
Bado yeye mwenyewe aridhie kuja Afrika, hivyo tujipe muda huenda CR7 anataka aweke rekodi ya kuchezea mabara yote
 
Unaelewa maana ya mkopo? Na usajili wa mchezaji usidhani analipwa tu na club...!
Ina maana atacheza Misri,ila Wasaudi ndio watakao mlipa kila kitu.....? au wewe mkopo kwenye mpira unavyojua wanamaanisha nini?

Halafu mkopo ni makubaliano,timu inayo mtaka inaweza ikamlipa full au ikagawana asilimia za kumlipa CR7 au may be ww unavyojua type ya contract ya CR7 na Al Ahly itakuwa ni ipi.
 
Back
Top Bottom