Tetesi: Al-Hilal kumsajili Cristiano Ronaldo kama mbadala wa Neymar baada ya majeraha yake kuleta sintofahamu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Majeraha ya mara kwa mara yanayomkumba nyota wa soka Neymar sasa yamezua sintofahamu kubwa juu ya hatima yake katika klabu ya Al-Hilal. Kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka Fichajes, klabu hiyo ya Saudi Arabia inaangalia uwezekano wa kumuuza mchezaji huyo wa Brazil ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu.
Pia, Soma:

+ Majeraha kumkosesha mamilioni ya Waarabu Neymar Jr, Al-Hilal kumvunjia mkataba mwezi Januari

Al-Hilal wanaripotiwa kuwa na hamu ya kumsajili mchezaji nyota wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, ili kuchukua nafasi ya Neymar. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno ameonesha uwezo mkubwa katika ligi ya Saudi Arabia na anapewa nafasi kubwa kama mbadala anayefaa kwa Neymar.
 
Hawa Al hilal hiyo ligi ya kwao wanataka wawe kama wamefunga nayo ndoa, kombe wanapata muda wowotr wakijisikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…