Al jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (umoja wa waislam wa tanganyika 19030s

Al jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (umoja wa waislam wa tanganyika 19030s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
AL JAMIATUL ISLAMIYYA FI TANGANYIKA (UMOJA WA WAISLAM WA TANGANYIKA) 1930s

Picha hiyo hapo chini inawaonyesha Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) wakiwa wamesimama mbele ya ofisi yao Mtaa wa Stanely na New Street (sasa Max Mbwana na Lumumba Avenue).

Wanasema picha inazugumza maneno elfu moja.
Wanasema jicho lako haliwezi kusahau kile jicho la camera iliona.

Siku chache zilizopita niliweka hapa picha ya jengo la shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika lililotaifishwa na serikali baada ya kuvunjwa EAMWS na kuundwa BAKWATA.

Waislam wameomba warudishiwe shule yao kwa kuwa waliijenga kama wakfu wamekataliwa.

Jengo hili ni mbele ya hapo ilipopigwa picha hii.

Katika picha hiyo ya Al Jamiatul Islamiyya kuna watu ambao wana historia za kusisimua sana.

Bahati mbaya sana hayakuweza kupatikana majina yote ya waliokuwa kwenye picha ila wachache hasa kwa kuwa picha ni ya zamani sana na si rahisi kutambua sura.

Lakini hapo hawawezi kukosa kuwepo Mzee bin Sudi na Ali Jumbe Kiro.

Al Jamiatul Islamiyya takriban wote ukimtoa Liwali Ahmed Saleh walikuwa wanachama wa African Association kisha TAA jina lilipobadilika mwaka wa 1948.

Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika yote ilijiunga na TANU pale chama kilipoasisiwa 1954 na Mweka Hazina wake Iddi Faizi Mafungo ndiye alikuwa pia Mweka Hazina wa TANU.

Hii ndiyo sababu ya hafla ya kumuaga Julius Nyerere safari ya kwanza UNO mwaka wa 1955 ilifanyika katika majengo ya shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Tuanze na Maalim Mohamed Matar:

Mwisho walio nyuma kushoto wa kwanza kapiga kilemba na kanzu ni Maalim Matar.

Nani Maalim Matar?

Maalim Matar alikuwa mwalimu wa kusomesha Qur'an na ndiyo aliyowasomesha wazee wetu wengi Qur'an hapo shuleni.

Mwanafunzi wake aliyekuja kuwa mtu maarufu sana ni Abdulwahid Sykes.

Maalim Matar alipata kuwekwa kizuizini mara mbili na kufungwa Ukonga, Dar es Salaam na Kiinua Miguu, Zanzibar kwa maonevu tu kwani hakupata katika maisha yake kujihuisisha na siasa.

Kassim Hanga aliporudi Tanzania akitokea Uingereza kwa Oscar Kambona na baada ya kuonywa akiwa London kuwa asirejee Tanzania na kukaidi na pia akaonywa bado akiwa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kuwa wala asithubutu kuingia mjini bali asubiri hapo hapo uwanja wa ndege arejee London na ndege hiyo hiyo iliyomleta na pia kukaidi, Ali Nabwa na huyo muonyaji wa Uwanja wa Ndege walimpeleka Hanga nyumbani kwa Maalim Matar akaombewe dua.

Maalim Matar watu wakimuheshimu sana kwa ucha Mungu wake na akiitadikiwa kuwa ni walii.

Kleist Sykes.

Yeye na Mzee bin Sudi ni waasisi wa African Association 1929 kisha Al Jamiatul Islamiyya 1933 wakiwa President na Secretary.

Ali Mwinyi Tambwe.

Ali Mwinyi Tambwe alikuja kuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya.

Ali Mwinyi Tambwe nilipofanya mahijianonae wakati wa kutafiti kitabu cha Abdul Sykes alinambia kuwa yeye ni mkubwa sana kwa Abdul na Ally Sykes na akiwaona wakija kusali Maghrib Msikiti wa Kitumbini na baba yao kawashika mikono.

Ally Mwinyi Tambwe anasema yeye alikuwa mkubwa na akii zake kamili.

Ally Mwinyi katika picha amekaa bega kwa bega na Kleist Sykes.

Picha hii ni ushahidi wa kauli yake.
Kwenye picha hiyo Abdul ni mtoto mdogo labda miaka 10 hivi.

Ally Mwinyi akiwa na Abdul Sykes alishiriki katika mazungumzo ya kumtia Julius Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA kwenye kikao kilichofanyika Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu mwaka wa 1953.

Kleist Sykes na mwanae Abdulwahid.

Hakika hawa hawahitaji kuelezwa kamwe.

Kleist Sykes kaacha mswada wa kitabu cha maisha yake na kutoka mswada huu ndiyo tumejifunza historia ya African Association na Al Jamiatul Islamiyya.

Abdul Sykes yeye maisha yake na ndiyo historia ya TANU yameandikwa na mwandishi.

Kitabu hiki ndicho kilichofunua mengi katika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuunganisha historia ya African Association na TAA 1929 - 1954 na historia ya TANU 1954 - 1961 uhuru ulipopatikana.

Mstari wa mbele katika picha wa tano kutoka kushoto ni Kleist Sykes akifuatiwa na Ali Mwinyi Tambwe kisha Liwali Ahmed Saleh.

Mstari wa katikati wa tatu kutoka kushoto ni mtoto Abdulwahid Kleist Sykes.

Ally Mwinyi alihusika sana katika harakati za kupindua serkali ya Mohamed Shamte Zanzibar mwaka wa 1964 na yeye ndiye aliyesaidia kuweka kambi maarufu ya Kipumbwi, Tanga iliyokuwa inawavusha Wamakonde kutoka mashamba ya mkonge ya Sakura kuingia Zanzibar mwaka wa 1961 kuipigia kura ASP na mwaka wa 1964 kushiriki katika mapinduzi.

PICHA: Maalim Matar, Mzee bin Sudi, Msafara wa TANU Zanzibar wakati wa kupigania uhuru Ali Mwinyi Tambwe (Ali Haluwa) wa kwanza kulia, jengo la Al Jamiatul Islamiyya na picha ya viongozi wa Al Jamiatul Islamiyya 1930s.

242799527_1030797007667677_8667500190440659172_n.jpg


Screenshot_20210924-220021_Facebook.jpg
 
Duh mzee sasa unakera relax kidogo.
Maana naona udini unakusumbua tu.
Relax Ok.
 
Kazi sana kulazimisha vitu ambavyo havina uhitaji..kubali tu wazungu walishateka mindinza watu..historia zao ndio zinatawala.

#MaendeleoHayanaChama
 
Duh mzee sasa unakera relax kidogo.
Maana naona udini unakusumbua tu.
Relax Ok.
Babu...
Siku zote ushauri wangu ni kuwa ikiwa hapendezewi na historia hii ya Tanganyika la kufanya ni kuacha kusoma post zangu.

Udini kuandika historia ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?
 
Kassim Hanga aliporudi Tanzania akitokea Uingereza kwa Oscar Kambona na baada ya kuonywa akiwa London kuwa asirejee Tanzania na kukaidi na pia akaonywa bado akiwa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kuwa wala asithubutu kuingia mjini bali asubiri hapo hapo uwanja wa ndege arejee London na ndege hiyo hiyo iliyomleta na pia kukaidi, Ali Nabwa na huyo muonyaji wa Uwanja wa Ndege walimpeleka Hanga nyumbani kwa Maalim Matar akaombewe dua.
Mzee Mohamed Said Said kwa ukarimu wako ikikupendeza naomba kujua msimulizi kuhusu maisha ya Kassim Hanga
 
Sipo huko ila nnapoona mtu kila akikaa kuandika mara abduli,ally,majid,hamza+++ ndo nachoka .kuna mambo mengi ya kutueleza kuliko kungangana na majina tu.
Mi msomaji wa mada za mzee siku nyingi ila naona inakuwa too much udini.
Babu...
Ikiwa ni historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika haya majina huwezi kuyaepuka.

Haya utayasoma hadi kiyama.

Wala kuwataja wapigania uhuru waliofutwa katika historia haijawa udini.

Ungejiuliza kwa nini Abdulwahid Sykes alifutwa kwenye historia ya TANU ilhali yeye na baba yake walihusika pakubwa katika TAA na TANU?

Ushapata kujiuliza?

Udini ni kuwapendelea watu wa imani yako ukapanga njama kuwahujumu wasio dini yako wakose elimu na fursa zote nchini.

Huu ndiyo udini.

Kwani kuna lazima kwako kusoma makala zangu?

Mbona ni jambo jepesi.
Pita wima usisome.
 
"Maalim Matar alipata kuwekwa kizuizini mara mbili na kufungwa Ukonga, Dar es Salaam na Kiinua Miguu, Zanzibar kwa maonevu tu kwani hakupata katika maisha yake kujihuisisha na siasa"


Mzee Mohamed

Unao Ushahidi hakujihusisha na siasa au umeamua tu kumtetea nduguyo?
 
Mzee Mohamed

It's really boring kuandika habari za udini kila siku huku ukipotosha historia ya nchi yetu kwa kukusudia

Ukweli watu wamekuchoka na hawakuamini japo unatumia nguvu kubwa kuwasadikisha

Nakushauri upumzike kuandika ili ujipe muda wa kutafakari njia zako
 
Mzee Mohamed

It's really boring kuandika habari za udini kila siku huku ukipotosha historia ya nchi yetu kwa kukusudia

Ukweli watu wamekuchoka na hawakuamini japo unatumia nguvu kubwa kuwasadikisha

Nakushauri upumzike kuandika ili ujipe muda wa kutafakari njia zako
Uzalendo...
Hii si udini hii ni historia ambayo ilifutwa.

Nimekaa kitako nikafanya utafiti na nikaandika kitabu ambacho sasa kipo toleo la nne katika miaka 23.

Ikiwa wewe unaona ni sawa kubaki na historia ile iliyoandikwa na Chuo Cha Kivukoni Cha CCM mwaka wa 1981 mimi sina neno lakini usiwe unakuja hapa kwa nia ya kunishambulia kwa kuandika historia ya wazee wangu.

Sidhani kama wewe unahusika na hili.

Mimi sijafanya ugomvi na wewe kwa kuamini historia ya Chuo CCM Cha Kivukoni .
Sasa nini kinakuchoma wewe kwa mimi kuandika historia hii iliyoweka ukweli wazi?

Kuhusu kupumzika.
Sijui inakuhusu nini mapumziko yangu?
 
"Maalim Matar alipata kuwekwa kizuizini mara mbili na kufungwa Ukonga, Dar es Salaam na Kiinua Miguu, Zanzibar kwa maonevu tu kwani hakupata katika maisha yake kujihuisisha na siasa"


Mzee Mohamed

Unao Ushahidi hakujihusisha na siasa au umeamua tu kumtetea nduguyo?
Uzalendo...
Bahati mbaya hukumjua Maalim Matar.
Hakuwa mwanasiasa hata kidogo.

Yeye alikuwa sufi.

Alipotoka jela siku moja akakutana na mtesaji wake jela aliyekuwa akimpiga Kiinua Mgongo bila sababu.

Wakati huo Karume alikuwa kesha kufa na wale waliokuwa chini ya mbawa zake wakawa hawana pa kwenda hoi hahe wanahangaika na dunia.

Basi Maalim Matar akamtolea salaam na aliona ile hali yake.
Maalim Matar alimwalika nyumbani kwake na akalanae chakula.

Haukupita muda huyu mtesaji akaugua akawa amelezwa hospitali.
Kuna jambo likawa linatokea la kusikitisha.

Huyu mtesaji akawa anapiga kelele usiku kucha na anakula kinyesi chake.
Ikabidi afungwe mikono na miguu kwenye kitanda chake.

Maalim Matar alipopata taarifa hii akaenda hopitali kumjulia hali.

Alikaa pembeni ya kitanda chake akanyanyanyua mikono yake akawa anaomba dua kwa Allah ampe mgonjwa yule shifaa.

Akawa kila siku anakwenda hospitali kumjulia hali yule bwana hadi alipofariki.

Maalim Matar nimemfahamu toka napata akili zangu na alimsomesha baba yangu Qur'an darasa moja na Abdul Sykes Al Jamiatul Islamiyya Muslim school 1930s.
 
Back
Top Bottom